Dstv Tanzania

VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WASHIRIKI MAZISHI YA MJUU WA DIWANI VITI MAALUMU TARAFA YA MALANGALI AVERINA MGAYA WILAYANI LUDEWA

Pichani ni katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwa na diwani wa viti maalimu Averina Mgaya.(Mfiwa)

Viongozi wa CCM mkoa wa Njombe, wameshiriki mazishi ya mjukuu wa diwani wa viti maalumu Avelina Mgaya, yaliyofanyika katika kijiji cha Madope Wilayani Ludewa

Kwa niaba ya chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe katibu wa siasana  mwenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amtoa rambirambi ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) na ameomba fedha hiyo akabidhiwe diwani huyo.



Katika salamu, amewaomba wanachi wa Ludewa kijiji cha madope  kuwa na makini na shughuri zote wanazofanya wakati wa kiangazi kwani wasipo kuwa makini wanaweza torosha moto na kuleta hasara kubwa katika jamii yako, haya ameyasema kutokana na uwekezaji walio uweka katika ardhi ya kijiji hicho.


Katika mazungumzo yake amewaomba vijana kufanya kazi kwa bidii kwani wasipofanya hivyo wajue ndoto ya kuwa  na maisha mazuri haipo tena, kwani hakuna njia nyingine ya kupata utajiri zaidi ya kufanya kazi kwa bidii. "Kwa kijana kuamka saa nne asubuhi ni aibu kubwa" Ngole amesema.

Na Erasto Kidzumbe 
0753580894





Hakuna maoni: