MKUU WA MKOA WA NJOMBE, CHRISTOPHER OLE SENDEKA AKISHIRIKIANA NA VIONGZOI WA CCM KUMALIZA MGOGORO WA BAJAJI NA HAISI NJOMBE MJINI
Na Erasto Kidzumbe
Mgogoro uliochukua takribani miaka mitano leo umepatiwa suruhisho,
kupitia tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa iliyoshirikisha SMATRA,Ofisi ya RPC,TANROAD na Mwanasheria wa Serikali.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewaomba madreva bajaji na haisi kufuata sheria za kuendesha vyombo vya moto ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima kwani sheria haipigiwi kura ni lazima.
Hatuwezi kulazimisha bajaji kufuata taratibu za haisi, watu wa bajaji watapewa vituo nane (8) vya maegesho na haitaruhusiwa kusimama kila mahali au kusanya abiria barabara kuu.Mkuu wa mkoa amesema yeye ni mzazi wa watu wote atahakikisha anatenda haki kwa watu wote ili wote waweze kupata kipato na kukidhi mahitaji ya wanachi kwa huduma zitolewazo na haisi na bajaji.
Vituo hivyo ni:
1.Ofisi ya CCM (W)
2.Ofisi ya Bank ya NJOCOBA
3.Duka la maziwa Njombe Mjini
4.Bank ya NBC Vituo viwili
5.Nationa Housing
6.Njiapanda ya NJOSS
7.Soko jipya la Dodoma.
Mkuu wa mkoa amepokea ombi la wananchi wa Njombe kuongeza bajaji ikiwa kama moja ya sehemu ya ajira.
Utoaji wa namba kwa ajili ya kupata bajaji mpya utakuwa ni wa haki kwa watu wote.
Pia amesema watakao pewa namba za kuongeza bajaji lazima wawe wananchi wa Njombe mji na si pahala pengine na ikibidi kuongeza bajaji fulsa hiyo itakuwa ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Na utaratibu huu hautaruhusu mtu mmoja kumiliki bajaji zaidi ya moja.
Pia amewambia wamiliki wa bajaji na haisi kuwa uongozi wa awamu ya tano haujaribiwi na mgomo wala maandamano
Amewambia madereva na wamiliki wa bajaji waendelee kutumia leseni hizo hizo ambazo walishalipia.
Utaratibu huu utaanza kufanya kazi mara moja ila ikumbukwe kuwa makubaliano haya sio msahafu au kuruhani hivyo yanaweza tokea mabadiriko muda wowote kwa utaratibu kama huu kwa manufaa ya kuboresha kazi.
Mwisho, Mkuu wa mkoa amesema Mh.Rais Dr.John Pombe Magufuri anatarajia kufanya ziara Njombe hivyo ameomba wananchi kujitokeza katika mkutano wake kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya katika mkoa wetu wa Njombe na Tanzania kwa ujumla
Rais ametoa fedha kiasi cha sh.bilion 220 za kutengeneza barabara toka Njombe mpaka Makete na zaidi Bilioni 150 kutengeneza barabara toka Makete mpaka Mbeya, alileta fedha zaidi ya Bilion 150 kupanua barabara toka Nyigu mpaka Igawa Mbeya, Pamoja na hayo mheshimiwa Rais ameshapata fedha kwa ajili ya kupanua barabara toka Makambako mpaka Songea.
Haya yote amefanya ndani ya Mkoa wa Njombe hii ni Neema kubwa ya Mkoa wetu wa Njombe.
Kwa mambo makubwa kama haya lazima Mh. Rais tumpongeze,tusiwe wanyimi wa fadhira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni