Dstv Tanzania

MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMEBE NJOMBE KUZUNGUMZA NA VIJANA WA GREEN GUARD MKOA WA NJOMBE







Mbunge wa Lupembe Joram Hongoli akiwa anapokelwa katika ofisi ya CCM Mkoa Njombe  na kukagua graride Greenguard Mkoa

Mbunge wa Jimbo la Lupembe amabaye ni katibu wa wabunge wa Mkoa wa Njombe Joram Hongoli amfika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Njombe kuzungumza na vijana ishirini na tatu wa Green Guard Mkoa, amekutana na viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe ambao ni Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike, Katibu wa siasa na ueuenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti, Ofisa wa UVCCM Mkoa wa Njombe Ndg, Choni, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Njombe Emmanuel Mlelwa




 Akikagua Greenguard Mkoa wa Njombe

Mbunge Joram Hongoli akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa Hosea Mpagike




 Mbunge akisalimiana na Katibu wa Siasa ana Uenezi Mkoa wa Njombe Erato Ngole
Vijana hao walikuwa wakipata semina elekezi ya kuwajengea uwezo wa  kujitegemea na ujasilianali ili kuweza kumudu mahitaji yao ya kila siku na kutambua fulsa walizo nazo katika mazingira wanaoyoishi, pamoja na hayo amewaomba vijana kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao.


 Mbunge Joram Hongoli  akitoa hotuba

Katika hotuba yake amesema kipimo cha utu wa mwanadamu ni kazi, na kama kuna mtanzania yeyote hafanyi kazi basi utu wake hauwezi kuonekana.

Hali kadharika amewapongeza vijana kwa kukitumikia chama cha mapinduzi ili kiweze kuendelea kuwatumikia watanzania na kuleta maendeleo ya watu wote.

Hata hivyo amewapongeza sana viongozi wa CCM kwa kuwatunuku vyeti vya utambulisho juu ya ushiriki wao wa semina elekezi na amewaomba wakawe mabalozi wazuri huko waendako



Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akimkabidhi cheti Mbunge ambacho kwa ajili ya kuwatununu Greenguard

Chama cha Mapinduzi kinatatua kero za watanzania wote bila kujali itikadi za vyama au ukabila na kinafanya haya kwasababu ya misingi ambayo chama hiki kimejiwekea.
Katika kuhitimisha  hotuba yake amewakumbusha utaratibu wa chama cha mapinduzi ni kuwa na Mwenyekiti na katibu wa CCM kuanzia kazai ya tawi hadi taifa, lakini chama kiliona ili kuweza kufanya kazi kwa urahisi na ufanisi ni lazima kuweka jumuiya mbali mbali  ndipo jumiya ya vijana ikazaliwa, kwani vijana ni tegemeo kwa kuwa ni taifa la leo na kesho. 

Mwisho amewambia safari ya uongozi huanzia Green Guard kwani viongozi wengi wa CCM ukiangalia historia yao inaonyesha walianzia greed guard na sasa wameshika nafasi kubwa katika chama  na wanafanya kazi kwa maadili makubwa kwani wanajua nini maana ya kuongozi.

Na Erasto Kidzumbe
0753580894 














Hakuna maoni: