CCM MKOA WA NJOMBE YAAMUA KUIBUA VIPAJI VYA MPIRA
Pichani ni Mgeni rasmi toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe akaizungumza na wachezaji ambao hawapo pichani
Ligi nyingine ya mpira iliyodhaminiwa na viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe imezinduliwa kata ya ramadhani
Ligi
hiyo imezinduliwa na Mgeni rasmi toka ofisa ya Mkurugenzi Halmashauri ya mji
Njombe katika kiwanja cha shule ya msingi kibena. Ligi hiyo inategemewa kuisha
tarrehe 04/11/2018
Wadhamini wa ligi hiyo ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa
Njombe Erasto Ngole, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Nehemia Tweve, katibu wa UVCCM
Wilaya ya Njombe Daniel Mhaza na Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Ramadhani
Michael Msigwa, Katibu wa hamasa na chipukizi Roberth Shejamabu na Comrade
Mtewele
Mgeni rasmi Ndg,Shengeru akisalimiana na Muamuzi wa mechi mbili zilizo fungua ligi ya kata ya Ramadhani
Katika
uzinduzi huo amewaomba vijana kucheza ligi hiyo ya mpira kwa upendo ili kuweza
kuishi katika misingi ambayo kananuni na taratibu za michezo ingependa wachezaji wawe hivyo.
Hata
hivyo amesema wachezaji wote wanategemewa katika taifa hili hivyo ni vizuri
kucheza mpira huku wakihakikisha wanakuwa salama kwani isipo kuwa hivyo yanaweza
potea malengo ya mtu katika mechi hizo.
Kazi inaendelea, muamuzi akimtabulisha makepteni wa timu mbili ili aweze kukagua wachezaji
Katika hobua yake amesema nchi yeyote ile duniani amabayo imeendelea inatumia nguvu kazi ya vijana, hivyo kama kijana unawajibu wa kujivunia na kusema wewe ni nguvu kazi ya nchi na nchi inakutegemea.
Pia
amehimiza michezo na kusema michezo kujenga uwezo mkubwa wa kuifiri na kufanya
maamuzi sahihi na haraka si hivyo tu pia hujenga afya, urafiki na ujirani mwema
Mwisho
amewapongeza viongozi wa CCM walioandaa ligi ya mpira na kusema hiki ndicho
chama chenye masikio makubwa kwani kila nyanza zote za maisha ukienda lazima
usikie CCM imefanya nini au inafanya nini.
Na
Erasto Kidzumbe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni