Dstv Tanzania

KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM MKOA WA NJOMBE YAFANYA ZIARA YA KIKAZI W-WANGING'OMBE YENYE LENGO LA KUIMARISHA JUMUIYA HIYO.

Katibu UVCCM mkoa wa Njombe Comrade Sure Mwasanguti akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji
Tanuru la kuoka viongozi (UVCCM), mkoa wa Njombe, wamewasili wilayani waging'ombe kwajili ya kuhakikisha jumuiya hiyo inakuwa imara. 

Ziara hyo ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ikiongozwa na mwenyekiti wake Ndugu Nehemia Tweve, katibu uvccm mkoa wa Njombe Comrade Sure Mwasanguti, katibu hamasa na chipukizi mkoa Johson Elly Mgimba, na katibu wa seneti mkoa wa Njombe Getruda..... wamewasili wilayani humo na kupokelewa na wenyeji wao wakiongozwa na mwenyekiti wao wa uvccm wilaya Ndugu Maiko Vidoga na wajumbe wake wa kamati ya utekelezaji. 
Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Wanging'ombe  Maiko Vidoga
Lengo kuu la Ziara hilo ni kuhakikisha jumuiya inakuwa imara katika nyanja ya mahusiano, uchumi, elimu na siasa.. ili kuhakikisha jumuiya inakuwa salama tayar kwa kuhakikisha usalama wa ccm na taifa zima ili kuhakikisha tunakuwa na viongozi imara kwa maslahi ya wananchi.

Katibu mtendaji wa wilaya hiyo ameweza kutoa taarifa ya kiutendaji na hali ya siasa wilayani humo ambapo taarifa ya hali kisiasa ni shwari licha ya kuwa changamoto hazikosekani na wanahakikisha wanakabiliana nazo, hali ya kiutendaji nayo ni shwari kwa kuwa ushirikiano ni mkubwa kwa viongozi wote wa matawi, kata wilaya na mkoa na jumuiya nyingine zote.

Akizungumza na vijana wa Wanging'ombe mwenyekiti wa jumuiya ya vijana mkoa wa Njombe amewataka vijana kuhakikisha wanakuwa na moyo wa kujitolea ndani ya ccm na  wanakazi kubwa ya kuhakikisha ccm inakuwa imara kwa maslahi ya taifa letu na kuwa kinara wa kuhakikisha amani inadumishwa ndani ya taifa letu kwa kupinga ubaguzi wa kila aina yoyote.
Katibu hamasa na chipukizi mkoa Johson Elly Mgimba
Pia amewataka kuhakikisha wanatumia vyema fursa zinazowazunguka ndani ya wilaya ili kujiimarisha vyema kiuchumi kwani anaamini endapo watakuwa na uchumi imara wataweza kukipigania chama bila kuteteleka, amewataka pia kuzitumia vyema 4% zinatolewa na halmashauri wazichangamkie kuzikopa kwa kuwa hazina riba hivyo watumie fursa hiyo kukopa na kuanzisha biashara ili kutimiza ndoto zao.
Pia  amewakumbusha pia rasilimali zilizopo wanging'ombe kama vile misitu, ardhi nzuri, utalii na kila aina ya mazao yanayopatikana huku vitumike kuwanufaisha na kuinuka kiuchumi kwani bila uchumi siasa hakuna ni ubabaishaji.

Naye mtendaji mkuu wa jumuiya hiyo comrade Mwasanguti hakuwa mbali na ujumbe wa mwenyekiti wake ingawa ameonekana kung'aka zaidi kwakuwa Yeye ndiye msimamizi wa kanuni amewataka wajumbe na wanachama kuhakikisha wanaheshimu taratibu zilizowekwa na uvccm kwani bila kuheshimu kanuni zetu tutakuwa hatuna nia njema na jumuiya yetu na taifa letu na bado tunawakosea wapiga kura wetu.


Huku katibu hamasa akipamba mashambulizi hayo kwakuwa piga jeki vijana wa wilaya hyo somo la uchaguzi wa chipukizi ndani ya wilaya hiyo na umuhimu wake ndani ya jumuiya hiyo na pia amewahimiza kufanya utafiti wa maendeleo ya jumuiya hiyo ili kuzidi kuboresha jumuiya yetu.


Kamati hiyo ya Utekelezaji imezitembelea kata za Ilembula na Malangali.

Zaidi Tazama Picha zote hapa

 

Hakuna maoni: