WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WANAOTARAJIA KUJIUNGA NA VYUO (M) MOROGORO WAANDALIWA SEMINA MAALUMU YA KUUFAHAMU UHALISIA WA MAISHA YA CHUO INAYOITWA “TWENZETU CHUO”
Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Fundisha Tanzania
Initiative (FTI) kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika Mkoa wa Morogoro
wameandaa Semina inayokwenda kwa Jina la “TWENZETU CHUO” ITAKAYO FANYIKA TAR
28/09/2018.
Semina hii imeandaliwa kwaajili ya Wahitimu wote wa Kidato
cha Sita wanaotarajia kujiunga na elimu ya
juu (Vyuo Vikuu) kwa mwaka huu 2018.
Imelezwa kuwa Semina hiyo itakuwa na lengo la kujadli
Fursa,pamoja na changamoto mbalimbali zitakaosaidia vijana hao kufanya vizuri
katika masomo yao,kuanzisha biashara pamoja na mambo mengine yanayohusu katika
maisha wawapo Vyuoni.
Mgeni Rasmi katika Tukio hilo atakuwa ni Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoa wa Morogoro Ndugu Ramadhani Salum Kimwaga.
Washiriki wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya
Tar 25/09/2018 na hakuna kiingilio cha
aina yoyote.
Semina hiyo itaongozwa na Wahamasishaji Mashughuli Tanzania akiwemo
Mjasiliamali MC Luvanda pamoja na
Livinus Nchimbi aliyewahi kuwa Raisi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM-DUCE) Mwaka 2016/2017 .
Kwa mawasiliano zaidi Wasiliana na Waaandaaji wa Semina hii
Muhimu Kwa Namba 0764158751 na
0684670440.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni