USHINDI HUU WA CCM UNATOA MAJIBU TISA YA MSINGI
Tumeshuhudia chaguzi ndogo za Mitaa, Kata na Majimbo zikiendelea tangu mwanzoni mwa mwaka jana 2017 mpaka sasa.
Kikatiba
chaguzi hizi zinatokana na sababu kadhaa ikiwemo Kifo cha kiongozi
katika nafasi husika, kujiuzuru, kufukuzwa uanachama, kiongozi
kuhukumiwa kwenda jela kifungo kinachoanzia miezi sita na zaidi na
muhusika kuugua ugonjwa wa akili (Ukichaa).
Chaguzi
hizi ndogo zote kuanzia 2017 Januari CCM imekuwa ikishinda kwa kishindo
ambacho haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mfumo huu wa Vyama
vingi, na hii imetupatia majibu tisa kutoka kwa wananchi kama
yafuatayo;
- Wananchi wamemuelewa sana Rais Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na hawapo tayari kumvunja moyo kwa kutoichagua CCM.
- Wananchi wameanza kutambua mbivu na mbichi, yaani ukweli na uongo (stori vijiwe na stori halisia)
-
Wanachi wameelewa mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM amabapo
yamekifanya Chama kuwa Chama Cha watu na kinachoshughulika na shida za
watu.
- Viongozi wa CCM wameelewa namna ya kufanya siasa, Nyakati, na Mabadiliko ya rika na Uelewa wa wananchi.
-
Viongozi wa Upinzani bado hawajaelewa washike hoja gani baada ya zile
za ufisadi, rushwa, Ndege, Urasimu, n.k kushughulikiwa vema na Serikali
ya CCM awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
- Wananchi wameelewa ni Chama gani chenye nia njema kwa Watanzania wanyonge kulingana na Itikadi yake, Sera, na Ilani yake.
-
Wananchi wameelewa ni Chama kipi ni Taasisi na Chama kipi ni mali ya
Mtu mmoja ama kikundi kidogo Cha Watu wenye maslahi binafsi.
-
Kwa kupima kauli za viongozi wa vyama mbalimbali, Wananchi wameelewa ni
wapi pakupeleka Changamoto zao na kushughulikiwa kwa urahisi na kwa
wakati.
- Wananchi
wanajua ni Ilani ipi inayoakisi matakwa yao hasa kiu walionayo kuifikia
Tanzania ya Viwanda ambayo ndio hasa msimamo wa Rais wa Tanzania na
Mwenyekiti wa CCM Ndg. John Joseph Pombe Magufuli.
Kuna
Mwanasiasa mmoja na msemaji wa Chama kimoja cha Siasa hapa Tanzania
aliwahi kusema " Vyama vya siasa ni kama nyumba ya vioo, kila
lifanyikalo ndani wananchi wanaona na kulifanyia tathimini, na matokeo
yao huwa ni kwenye sanduku la kura". Hivyo kinachoendelea sasa ndio
majibu ya wananchi dhidi ya matendo ya ndani ya Vyama vya Siasa.
Mwandishi: Said Said Nguya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni