VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAZINDUA LIGI NYINGINE YA MPIRA ILIYODHAMINIWA WA KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE
Viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe wa wamezindua ligi ya
mpira katika jijini cha lwangu kata ya kifanya, ligi hiyo imedhaminiwa na Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe. Katika
uzinduzi huo Katibu wa Siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole ameambatana
na viongozi wa mkoa ambao ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve,
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti, katibu wa Jumiya ya wazazi Mkoa
wa Njombe Lucas Nyanda na afisa mmoja wa UVCCM Mkoa wa Njombe ndugu Choni.
Katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe amewaomba vijana wa
kijiji cha lwangu kushiriki ligi hiyo kwa kuzingatia nidhamu ya hali ya juu ili
kuweza kufikia malengo ya kuanzisha
ligi, malengo hayo ni kujenga udungu, ujirani mwena na kufahamiana baina ya
vijana wanaoshiriki ligi hiyo toka vijiji kumi na sita vya halmashauri ya mji
wa Njombe.
Pia katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe amepata fulsa ya
kuwasalimu na kuzungumza na vijana wa
kijiji cha lwangu na kifanya ambao mechi zao zimeshiriki kuzindua ligi hiyo,
amewaasa na kuwambia vijana wanawajibu wa kupendana na kuheshimina ili kuweza
kufanikisha ligi hiyo, pili amesema hata kuwa tayari kuona amani inatoweka
katika ligi hiyo iliyoanzishwa kwa madhumini ya kujenga undugu na kuimalisha
juiya ya vijana.
Hata hivyo Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe
ambaye ndie mgeni rasmi amefurahishwa na mwitikio wa vijana katika ligi hiyo. Amewambia ligi hii haitakuwa ya muda bali
itakuwa ni ligi ya kudumu, katika ligi hiyo amewambia mshindi wa kwanza
atazawadiwa kiasi cha shiingi laki tatu (300,000/=) na mshindi wa pili
atazawadiwa kiasi cha shilingi laki mbili (200,000/=), pia amewaomba waamuzi wa
ligi hiyo kufanya uamuzi wenye haki na kweli ili mshindi atakayeshinda awe
mshindi wa kweli mbele za Mungu na mwandamu.
Katika uzinduzi wa ligi hiyo timu iliyoshinda ambayo
inatoka kijiji cha kifanya imezawadiwa kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000/=)
kama pongezi katika uzinduzi huo wa ligi na kushinda katika mechi hiyo, pia
timu ya lwangu nayo imezawadiwa kiasi cha shiringi elfu therathini
(30,000/=) kama pongezi kucheza mpira
kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu.
Pia amewambia vijana CCM, imeshuka kushirikiana na
wanachi katika nyanja zote za maisha ambazo ni kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mwisho amewaomba vijana na wanachi kwa ujumla kuendelea kukiamini chama cha
mapinduzi kwani ndicho chama kinacho wapenda na kuwajali watanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni