Dstv Tanzania

KATIBU IDARA YA VYUO NDG. KHAMANA SIMBA AKUTANA NA VIONGOZI WA SENETI YA VYUO (M) DAR ES SALAAM

Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Comred Khamana Juma Simba amezungumza na Viongozi wakuu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam leo Ofisi ndogo za Makao Makuu UVCCM Upanga Dar es Salaam.


Mkuu huyo wa Idara amewataka Viongozi wote wa Seneti kujali maslahi ya Vijana wote vyuoni na kutumia fursa walizonazo kuisaidia Serikali katika kutimiza matamanio yako. 
Aidha, Ndugu Khamana amesisitiza na kuomba Ushirikiano wa Viongozi wa Seneti huku akiwasihi kuitumia Ofisi ya Idara hiyo kwani ni yao na ndio sehemu sahihi kwao kujiuliza na kupata masuluhisho ya Changamoto mbalimbali zihusuzo Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu nchini.

Hakuna maoni: