KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ASHIRIKI BARAZA LA UVCCM MKOA WA NJONBE,UVCCM WAMTUNUKU HATI YA PONGEZI KWA KUTAMBUA MCHANGO WAKE.
Katibu wa siasa na unenzi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akizungumza na wajunbe wa baraza kuu la Vijana mkoa wa Njombe. |
Katika mazungumzo hayo amesema yeye ametoka katika jumuiya ya vijana na anawapenda sana vijana na hata acha kuwapenda vijana wa jumuiya hiyo ya vijana.
Katiba mazungumzo hayo ametoa zawadi ya mpira mmoja mmoja Kwa UVCCM Kila Wilaya wenye thamani ya shilingi laki moja 100,000/= na kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kama fedha ya chakula kwa kila wilaya isipo kuwa wilaya ya Njombe wamepewa mpira mmoja tu.
Pia amewaasa vijana walioaminiwa na chama na serikali kuwa watu wenye kuitambulisha Njombe kwani vijana wasipo fanya hivyo watafanya vijana wengine wakose fulsa.
Katika baraza hilo, jumuiya ya vijana wamemtunuku cheti cha utumishi bora kwani amekuwa ni kiongozi bora kwa kuisaidia juiya ya vijana na kujitolea pale wanapo hitaji msaada wa kuhakikisha jumuiya hiyo inasimama na juweza kujitegemea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni