Dstv Tanzania

KATIBU WA CCM MKOA WA NJOMBE HOSEA MPAGIKE AENDESHA SEMINA YA UONGOZI NA MAADILI KATIKA BARAZA LA VIJANA UVCCCM MKOA WA NJOMBE


Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike akitoa semina ya uongozi na Maadadili katika baraza la umoja wa UVCCM Mkoa wa Njombe, katika semina hiyo ameanza kwa kutoa maana halisi ya kiongozi na maadili.

Amesema moja ya sifa kiongozi ni mtu aliyetosheka (kuridhika na kile anachokipata)

Sifa ya pili,awe mtu anayeweze kueneza matunda ya uhuru kwa maslahi ya watu wote.

Tatu, asiwe mtu mwenye upendeleo

Nne,  Asiwe mtu wa kutoa na kupokea rushwa 

Maadili kwa kijana anatazamwa katika uzalendo wa nchi yake kwa mujibu wa kanuni ya jumuiya ya vijana.

Uzalendo kwa mujibu kwa kanuni ya umoja wa vijana ni ujasili  alionao kijana juu ya nchi yake.

Katibu CCM mkoa wa Njombe amewaasa vijana kutotangaza wanataka kufanya nini bali watangaze nini wamefanya kwani mpango kazi ni siri.

Pale mwanachama anapokisaliti chama,chama cha mapinduzi kina utaratibu wa kutoa adabu na adhabu hizo zipo sita.

1.Onyo
2.Onyo kali
3.Kalipio
4.Kuvuliwa uanachama
5.Kuvuliwa uongozi
6.Kufukuzwa uanachama
Amesema chama cha mapinduzi ni chama madhubuti ambacho kimejiwekea utaratibu mzuri kwa kujiongoza.

Pia amesema kama viongozi ni lazima kuwa na malengo kwa hakuna maendeleo yanayoweza kuja bila ya kuwa na malengo, hata hivyo amewaomba viongozi wa jumuiya kuheshimiana kwani bila kuheshimiana hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana.


Mwisho ametoa pongezi kwa Thito Nichoraus Stambuli kwa kuteuliwa kuwa katibu tarafa kwani amekuwa kijana mchapa kazi na mvumilivu katika chama cha Mapinduzi.

Hata hivyo ameomba Stambuli akawe mjumbe mzuri na akafanye kazi kwa bidii kama alivyokuwa akifanya katika chama cha mapinduzi.
Pia amempongeza Omega Thobias kuteuliwa kwenda makao makuu ya CCM kwenye kitengo cha Hamasa, Chipukizi ,   Masiliano na Utafiti.

Mwisho amewashukuru viongozi wa jumuiya ya vijana kwa kutambua mchango wake katika jumuiya ya vijana na kuamua kumtunuku cheti cha uongozi uliyotukua kwani utakuwa ukumbusho mzuri na waheshima katika katika historia ya uongozi wake.

Na Erasto Kidzumbe
0753580894

Hakuna maoni: