KIKAO CHA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA NJOMBE NA WAJUMBE WA BARAZA LA JUMUIYA HIYO
Na Erasto Kidzumbe
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akizungumza na wajumbe wa baraza mkoa wa Njombe, akiambatana na katibu wake Sure Masanguti,Mjumbe wa baraza kuu Thobias Omega na katibu hamasa Mkoa wa Njombe, Johnson Mgimba, Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike na Katibu wa siasa na uenezi comred Erasto Ngole
Katika baraza hilo amesema anatarajia kufanya kambi la Green guard la mkoa litakalo kusanya vijana sita 6 kila wilaya na kuleta jumla ya vijana 24 na kambi hilo litafanyika kuanzia tarehe 22 mpaka tarehe 26 mwezi wa tisa mwaka 2018.
Amesema lengo la kufanya kambi hilo ni kuhakikisha anapata green guard wazalendo na wenye mapenzi mema na chama na uwezo wa kukitetea chama cha mapinduzi kwa hali na mali.
Hata hivyo amesema Moja ya changamoto wanayokutana nayo viongozi hawa wa Jumuiya ya vijana ya mkoa wa Njombe ni kukosa usafiri, kwani muda mwingi wamekuwa wakitumia gari la kuazima kwa Mwenezi wa Mkoa na jumuiya nyingine.
Amewaomba wajumbe hawa wa Baraza kuhakikisha ajenda hii ya kununua gari
inawagusa vichwani mwao ili kuweza kujinusuru katika changamoto hiyo.
Nje na ajenda hiyo amesema baadhi ya kamati ambazo ziliundwa na baraza na hazifanyi vizuri katika majukumu yake kamati hizo zitavunjwa na kutafuta wajumbe wa kamati wenye nia nzuri na mapenzi mema na chama.
Pia mwenyekiti amesema makatibu hamasa na chipukizi wa Wilaya wameongezewa majukumu ambayo ni Mawasilianao na utafiti. Hata hivyo amewataarifu kuwa kuanzia sasa makatibu hamasa na chipukizi wa Wilaya watakuwa wajunbe waalikwa wa baraza la mkoa la UVCCM.
Mwisho amesema makatibu wote wa wilaya wakafungue bank za wanachama (Taarifa za wanachama ) wote na kuhakikisha taarifa hizo zinafika katika ofisi ya vijana mkoa wa Njombe
Katika kikao hicho katibu wa siasa na uenezi mkoa Njombe amepewa nafasi na kuzungumza na wajumbe hao wa baraza, katika mazungumzo hayo amewapa fursa nyingine nje na parachichi ni kulima pasheni kwani pasheni inafaida mara mbili ya parachichi, hivyo amewashauri vijana wajikite katika kilimo hicho ili kuweza kujinusuru na unyonge wa kiuchumi.
Matharani mwenezi amempongeza Omega Thobias kwa kuteuliwa kwenda makao makuu ya CCM katika kitengo cha hamasa, chipukizi, mawasiliano na utafiti.
Baraza la UVCCM Mkoa wa Njombe limesikitishwa sana na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Njombe kwa kutoshiriki vikao mara zote, pili mwenyekiti huyo kujiingiza na kuwa mmoja wa mtia sahihi wa akaunti ya jumuiya ya vijana ikiwa ni kinyume na kanuni.
Kwa kuhitimisha baraza la UVCCM Mkoa wa Njombe kupitia mwenyekiti wao amesema, kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake pamoja na tuhuma nyingi dhidi yake na malalamiko ya kamati ya utekelezaji ya Wilaya ya Njombe juu ya mwenyekiti huyo, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe metangaza rasmi kuwa kuanzia leo tarehe 14/09/2918 baraza halimtambui tena Devotha Steven Kioko kama mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Njombe. Pia Mwenyekitia wa UVCCM Mkoa wa Njombe ameagiza apewe barua mara moja ya kusimamishwa uongozi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazo mkabili hadi pale uchunguzi utakapo kamilika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni