KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AZUNGUMZA NA WAJASIRIMALI WADOGO KIKIJINI KWAKE ITULIKE.
Na Erasto Kidzumbe
Leo mapema kabisa, Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwasalimia vijana wa kijijini kwake Itulike.
Katika salamu zake amesema amefurahishwa na jitihada wanazofanya vijana hao za ujasilimali mdogo mdogo kwani huwaingizia kipato cha kufanya waweze kumudu kupata mahitaji yao ya kila siku kuliko kuwa vijana wa kukaa magengeni na kujadili mambo yasiyo na tija katika taifa hili.
Katika salamu zake amewambia hakuna maendeleo yanayoweza kuja kirahisi rahisi kwani suala hilo linahitaji kujituma,nidhamu ya fedha na uthubutu.
Vijana hao wamefurahi kwani amekuwa akiwatia moyo na kuwapa mbinu mbali mbali za kuweza kujipatika kipato halali ili kuweza kuendesha maisha yao kiurahisi.
Pia amesema hatasita kuwambia ukweli pale wanakapokuwa wanakosea kwani duniani hapa hakuna mtu asiyependa kuwa na maisha mazuri na maisha mazuri hakuna mtu wa kukutengenezea zaidi ya jitihada zako mwenyewe.
Mwisho amewaomba vijana hao waendelee kukiamini chama cha CCM kwani ndicho chama pekee Tanzania kinachoweza kuwaletea maendeleo Watanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni