UMOJA WA VIJANA CCM MKOA WA NJOMBE WAANDAA KONGAMANO KABAMBE LENYE LENGO LA KUIBUA NA KUZITUMIA FURSA ZA KIUCHUMI KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA.
Na.Erasto Mgeni.
Umoja wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Umeandaa Kongamano la Wajasiliamali
litakalofanyika Siku ya Tarehe 14/09/2018 katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi
Uliopo katika kata na Mtaa wa Mji Mwema Mjini Njombe.
Katika Taarifa Iliyotolewa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe
Ndg Sure Mwasanguti imesema Kongamano hilo litafanyika kuanzia Majira ya Saa 3:00 Asubuhi .
Mwasanguti amewakaribisha Vijana wote wa Mkoa wa Njombe Kushiriki
Kongamano hilo ambalo limelenga
kubadilisha Maisha ya Vijana Kiuchumi.
Akizungumza na Stambuli Media Mwasanguti amesema Lengo la
Kongamano hilo ni Kuhakisha Kama Umoja wa Viajana Mkoa wa Njombe wanakuwa na
Mkakati wa Pamoja wa kutumia fursa
zilizopo mkoani humo ili kwenda sambamba na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano
ya Kuwa na Uchumi wa Kati Kwa kujenga Viwanda.
“vijana wote mnakaribishwa na lengo letu ni kuhakikisha
tunakuwa na mkakati wa pamoja wa kutumia
fursa zilizopo mkoani Njombe kuelekea uchumi wa viwanda”amesema Mwasanguti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni