Dstv Tanzania

LIGI YA MPIRA “SADOCK MWANDA CUP” YAHITIMISHWA WASHINDI WATUZWA DONGE NONO.


Na.Erasto Mgeni.

Hatimaye Ligi ya Mpira ya kinyang’anyiro cha Kikombe La  “SADOCK MWANDA CUP”iliyorindima Tangu mwezi wa 7 katika kata ya Halungu   Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe Imehitimishwa leo na Washindi kuondoka na Zawadi Nono.

Ligi hiyo ambayo ilifadhiliwa na Kada maarufu Kutoka Songwe Bwana Sadock Mwanda ilishirikisha Timu 38 ambao katika timu hizo timu ya kwanza iliyoibuka na Ushindi ni Timu ya wataalamu kutoka Lwati,iliyoshika nafasi ya Pili ni Comandoo kutoka Shasya na ya Tatu ni Simotwiga  kutoka Halungu.

Katika Hafla ya Kukabidhi ushindi wa Timu zilizofanya Vizuri Mgeni Rasmi alikuwa ni Bwana Lazima Simbeye,shughuli ambayo ilisindikizwa na Burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii na Vikundi vya Ngoma za Asili.

Akizungumza na Mtandao huu Bwana Sadock Mwanda amesema kufanyika kwa ligi hiyo ni sehemu ya kukuza  vipaji vya vijana katika Soka huku akiwataka Vijana kuendelea kushiriki vema katika Michezo.
Mshindi wa Kwanza ambaye ni Timu Kutoka Lwati amekabidhiwa kitika cha Tsh 150,000/=,Mshindi wa Pili ambaye ni ni Comandoo kutoka Shasya amekabidhiwa 100,000/= na mshindi wa tatu Simotwiga  kutoka Halungu amekabidhiwa 50,000/--

Katika Hafla hiyo Kikundi cha Ngoma kilichosherehesha Kimepewa Shilingi Elfu 60 pamoja na wasimamizi wa watu waliopewa Shilingi elfu 30.

Hakuna maoni: