TANZANIA YA VIWANDA IKO WAPI?
Mara
kadhaa baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza, TANZANIA YA VIWANDA IKO
WAPI? Leo nitawaletea makala fupi inayoelezea na kutaja baadhi tu ya
viwanda vikubwa vilivyojengwa kati ya 2016 - 2018 ili kujibu swali hilo,
Kwa kuwa tunajukumu la kuwasaidia ili wasiangamie kwa kukosa maarifa.
Nitaeleza orodha ya Mfano ya viwanda vilivyoanzishwa katika muda wa
miaka miwili na nusu ya Rais John Pombe Magufuli.
-
Mlandizi Mkoani Pwani kimejengwa kiwanda kikubwa cha Chuma kinachoitwa
Kiluwa Steel Group ambacho kwa sasa kinauwezo wa kuzalisha tani
1,200,000 za nondo kwa mwaka. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Mtanzania
Bw. Mohamed Said kwa 51% na 49% zinamilikkwa na muwekezaji kutoka China.
Kiwanda kimezinduliwa tarehe 21 Juni, 2017.
-
Huko Kibaha Mkoani Pwani kimejengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza
vifungashio cha Global packaging Tanzania Ltd chenye uwezo wa
kutengeneza mifuko ya sandarusi 53,000 kwa siku. Hii ni kwa ajili ya
kuhifadhia mazao kama mahindi, Mtama na nafaka zingine. Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Mtanzania Bw. Joseph Wasonga na kimejengwa kwa gharama
ya sh. Bilioni 8.
-
Kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato Jijini Mwanza
kilichojengwa na Kampuni ya kitanzania ya Moitsan ambapo kimegaharimu
sh. Bil. 11. Kinauwezo wa kuzalisha Chupa 1,200 kwa dakika moja na
kitaungana na kiwanda kama hiko kilichopo Mkoani Pwani na kwa kiasi
kikubwa kitasaidia sana kuongeza tija katika mazao ya matunda kanda ya
ziwa na Pwani.
- Kiwanda
kikubwa cha kusindika na kuzalisha mafuta ya alizeti cha Mount Meru
Millers kilichopo mkoani Singida. Kiwanda hiki kinauwezo wa kuzalisha
tani elfu 90 za mafuta ya alizeti kwa mwaka. Kiwanda hiki kitachochea
zaidi ulimaji wa mazao ya alizeti na kuongeza tija kwa wakulima hasa
Mikoa ya kanda ya kati.
-
Kiwanda kikubwa cha Dawa za binadamu kilichojengwa Buhongwa Mwanza cha
Prince Pharmaceutical. Kiwanda hiki kimegharimu sh. Bil. 20, hivyo
kurahisisha upatikanaji wa madawa Mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na
Kagera. Hiki ni kiwanda cha tano cha madawa ya binadamu hapa Tanzania
vilivyojengwa awamu hii ya tano. Hiki kimezinduliwa mwezi Mei 2018.
-
Kiwanda cha kutotoresha vifaranga na kuzalisha vyakula vya kuku cha
Silverland kichopo Ihemi -Iringa. Kiwanda hicho kinauwezo wa
kutotoresha vifaranga 150, 000 kwa wiki na Tani elfu 40 za chakula cha
kuku kwa saa, mwaka huu pekee wameuza vifaranga 7,200,000 ndani na nje
ya nchi zikiwemo nchi za Ethiopia, Kenya, Nigeria na Uganda. Kiwanda
hiki kimezinduliwa Mwezi Mei, 2018.
-
Huko Chalinze na Mkuranga Mkoani Pwani vimejengwa viwanda vikubwa vya
vigae (Tiles) na kampuni za Twayford Tanzania Cereramics na Goodwill
Ceramics Tanzania Ltd huko Mkurunga vyenye uwezo wa kuajiri wafanyakazi
takribani 9000 rasmi na ajira za muda na kushusha zaidi gharama za
ujenzi.
- Ukamilifu wa
kiwanda kikubwa cha Sigara mkoani Morogoro cha Philips morris
International kwa shilingi Bilioni 65. Kiwanda hiki kinauwezo wa
kuzalisha sigara Milioni 400 na kulipa kodi ya sh. Bilioni 12 kwa mwaka
ambapo kimeajiri Watanzania 520.
Hivyo
ni baadhi tu ya viwanda vilivyokwisha jengwa na kuzinduliwa kati ya
viwanda 2530 katika awamu hii ya tano ya Serikali ya Rais John Pombe
Joseph Magufuli.
Tanzania ya Viwanda sasa ni dhahiri.
Na mwandishi wetu
Said Said Nguya
0658354328
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni