KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE AIONGEZEA NGUVU HALMASHAURI KUU CCM LUDEWA, WAKATI WA KUWASILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole, (wa pili toka Kushoto ) amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ludewa (aliyesimama kushoto) Comrad Andrea Kisele kiasi cha shilingi laki tano 500,000/= kwa ajili ya posho za wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Ludewa.
Hata hivyo katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe amewapongeza viongozi wa CCM wa Wilaya Ludewa kwa ujenzi wa chama, kwani wamekuwa wakijitoa na kujituma katika shughuli za chama.
Pia amempongeza Mkuu wa wilaya kwa ushirikiano anaoutoa katika kujenga chama mapinduzi, kwani amekuwa kiungo mzuri baina ya chama cha mapinduzi, Serikali na wanachi wa Ludewa.
Mwisho amewaomba wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ludewa kumtumia vizuri Mkuu huyo wa wilaya kwani ni msaada mkubwa katika chama cha mapinduzi.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni