Dstv Tanzania

LIGI YA MPIRA ILIYOANDALIWA NA KATIBU WA SIASA NA UNEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE YAZINDULIWA RASMI

Na Erasto kidzumbe

Ligi ya katibu wa Siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole imezinduliwa leo na mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akiongoza na katibu wake wa UVCCM Sure Masangu, afisa wa UVCCM mkoa  ndugu Choni na Katibu wa Jumuiya ya wazazi bwana Lucas nyanda.

Ligi hiyo itahusisha matawi matatu ya UVCCM yanayo patikana katika kijiji cha itule na matawi hayo ni Maheve,Amani na Shuleni.

Ligi hiyo inashindaniwa shilingi laki tano 500,000 iliyotolewa na Katibu wa siasa na uenezi, na fedha hiyo imeshakabidhiwa kwenye tume inayo endesha ligi hiyo. 

Katika wakati fedha hiyo inakabidhiwa mwenezi amesema anaomba fedha hiyo itolewe kwa mshindi atakayeshinda kutokana na uamuzi wa tume iliyopewa dhamana ya kusimamia ligi hiyo,

Mwenezi anafanya hivyo ili kuweka usawa kwani moja ya tawi linaloshindania fedha hiyo linatoka katika mtaa anao ishi mwenezi hivyo ili kuepuka lawana na kutenda haki ni vema kuunda chombo kitakachotenda haki ili ligi hiyo iwe ya kweli na haki.

Wakati wa uzinduzi mgeni rasmi ambaye bi mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa njombe, amsema michezo sio adau ila ni urafiki hivyo lazima vijana kulijua hilo ili kuepuka ugomvi uso wa lazima.

Hata hivyo mwenyekiti amewaomba vijana kuna na nidhamu wakiwa katika mashindano hayo ili kufikia dhima ya ligi hiyo na wasipo fanya inaweza kutokea ligi hiyo isiishe kwa sababu ya kushindwa kuwa na heshima kwa mtu akikosa heshima anaweza kufanya mambo ambayo yatafanya watu wakoseimani kwa kijana




Hakuna maoni: