Dstv Tanzania

UVCCM LUDEWA WAWEKA MEZANI MIPANGO YA UIMARISHWAJI WA JUMUIYA NA UCHAGUZI WA CHIPUKIZIWAKUBALIANA KUPIGANIA UCHUMI WAO KWA KUANZISHA MIRADI MIKUBWA YA KIUCHUMI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Ndugu Bi. Theopister Mhagama ameongoza Kikao cha Baraza la UVCCM Wilayani humo lililofanyika kwa malengo ya kujadiliana uhai wa jumuiya na kwa jinsi gani UVCCM Ludewa inaweza komboka kiUchumi. 

Akiwa karibisha Wajumbe kwenye Baraza hilo Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Hassan Kapollo aliwasisitiza Vijana kuangalia zaidi Ustawi wa Uchumi wa Jumuiya na sio kujadiliana mambo ambayo yatakuwa hayana tija kwa Jumuiya. 

Mwenyekiti Theopister alisema, "Ndugu Vijana wenzangu wana Mapinduzi, natambua na mtakumbuka wakati wa Ziara yangu kwenye Kata zenu Changamoto yetu kubwa ni ukosefu wa Uchumi Imara na sasa ni wakati wetu kukua kiUchumi.. ".  Mwenyekiti ameelezea jinsi ambayo Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na mikopo ya Serikali huku akiwataka Vijana waishio mwambao wa Ziwa Nyasa kujikita katika uzalishaji wa samaki na uvuvi. 
Baraza la Vijana wa Ludewa limekubaliana kwa pamoja kupigania Uchumi wao na kuadhimia kujenga Vibanda 10 vya biashara vitakavyokuwa vikipangishwa na kuiingizia Jumuiya mapato. 

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Bakari Mfaume ambaye ndiye Mlezi wa Jumuiya hiyo amewakanya Vijana kuwa Wazalendo na wenye kujali Utu baina yao na kwa watu wote kama jamii iwazungukayo. Aidha, Wajumbe wameombwa kujiandaa na Zoezi la Uchaguzi wa Chipukizi ambalo lishapangwa kuanza kufanyika ndani ya muda mchache ujao.

Hakuna maoni: