Rais Magufuli Asema Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka Ndo Anayeongoza Kwa Kuchapa Kazi Vizuri Tanzania Nzima
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtaja
mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, kuwa ndiye mkuu wa mkoa kinara
anayepiga kazi na kwamba hana mfano licha ya kupuuzwa kabla hajamteua.
Hayo
ameyasema leo mkoani Simiyu wakati akihutubia wananchi wa mkoa huo
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya siku 7 katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa, wakati anajaribu kutafuta wakuu wa Wilaya na
wakuu wa mikoa aliambiwa na vyombo vyake kuwa Mtaka hafai hata U-DC
lakini yeye akaamua kumteua kuwa mkuu wa mkoa kwasababu anajua watu
wazuri huwa wanapingwa vita sana.
''Nilipotaka
kumteua niliuliza vyombo vyangu nikaambiwa hafai kabisa lakini
nimeuliza ripoti ya Wakuu wa Mikoa wanaofanya kazi vizuri, wakaniletea
Mtaka ndio namba moja na namba mbili ni yeye kwa kifupi hana mfano'',
amesema.
Aidha
Rais Magufuli ambaye atakamilisha ziara yake katika mikoa hiyo siku ya
Jumatatu Septemba 10, 2018 amemtaka Mtaka kuendelea kuchapa kazi wala
asiyumbishwe kwasababu yeye anajua watu wanaopigwa vita na kuwekewa
maneno ya ajabu ndio wazuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni