Dstv Tanzania

MWENYEKITI UVCCM MKOA WA NJOMBE NEHEMIA TWEVE AWAJENGA UWEZO VIONGOZI WA MATAWI YA KATA YA RAMADHANI MJINI NJONBE

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wanJombe Nehemia Tweve Akizungumza na Vijana na Viongozi wa UVCCM Kata ya Ramadhani Ambao hawapo Pichani
Na Erasto Kidzumbe


Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoa wa Njombe Ndg.Nehemia Tweve amewaeleza  viongozi wa matawi dhamana walionayo katika jumuiya hiyo ya vijana na chama kwa ujumla.

Amewaleza kuwa vijana ndio jeshi kubwa linalo tegemewa katika chama ndio maana hata mheshimiwa rais anawapa vijana dhamamana kubwa ya uongozi katika chama na serikali kwa ujumla na jambo hili vijana wanawajibu wa kulitambua na kulilinda kwa gharama yeyote kuhakikisha wanaaminiwa zaidi na zaidi.

Katika mazungumzo yake amesema ni lazima kijana ahakikisha chama cha mapinduzi kinaendelea kushika dola milele na milele kwani ndicho chama chenye uwezo wa kutatua kelo za wananchi hasa watanzania.

 Katika mazungumzo yake amesema lazima mitaa yote iliyoenda kwenye chama cha upinzani irudi CCM kwani mitaa yote ilioko upinzani hakuna kinachofanyika zaidi ya midahalo isiyo na mwisho huku watanzania waliowapa dhamana wakiendelea kupata tabu.
Pian amesema anahitaji kuona viongozi waunganisha watu na sio kutengeneza makundi kwani umoja ni nguvu.

Hata hivyo amewakumbusha vijana na kuwa muda wa uchaguzi umekaribia hivyo tunawajibu wa kujithimini namna ya kushiriki uchaguzi huo.

 Mwenyekiti pia amewapongeza vijana wa CCM wa ramadhani kwa kufanya vikao ili kuweza kujengana na kushauriana namna ya kuifanya jumuiya izidi kwenda mbele kwani jumuiya iko salama kuliko hata inavyofikiliwa.


Angalia picha zaidi

Hakuna maoni: