Dstv Tanzania

MBUNGE WA JIMBO LA MANONGA MH. SEIF KHAMIS GULAMALI AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MIRADI INAYOTEKELEZWA JIMBONI KWAKE.

Mh. Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa jimbo la Manonga amefanya ziara kujionea maendeleo ya miradi inayotekelezwa jimboni kama vile;-

Kituo cha Afya Simbo

Ujenzi wa Madarasa matatu, katika shule ya sekondari Mwisi



Pia amepita na kukutana na kamati ya Zahanati ya  Nkinga, Viongozi wa CCM na wadau wengine.

Haitoshi, mbunge ameahidi kutoa Tsh. 430,000 kwa ajili ya kuvuta maji ya Uhakika kwenye Zahanati ya Nkinga.

Ameahidi kuongeza vitanda viwili vya kujifungulia.

Jioni hii, Mbunge amefanya kikao na wachezaji pamoja na Uongozi wa timu yetu ya Manonga Queens ambayo jana tu iliishinda Singida Worrier kwa goli mbili. Mh. Gulamali amekabidhi mipira miwili. 

Pia ameahidi jezi na vifaa vya michezo ambavyo ameshaviagiza kwa ajili ya timu hii itakayouwakilisha mkoa mzima wa Tabora kwenye michuano ya soka daraja la kwanza Tanzania kwa timu za wanawake.


Hakuna maoni: