Dstv Tanzania

UVCCM WILAYA YA MUFINDI YAFANYA BARAZA

Umoja wa vijana wilaya ya mufindi chini ya mwenyekiti wake ndugu Christian Mahenge na katibu wake ndugu Hassan Kindamba wamefanikiwa kufanya baraza la wilaya kwa mujibu wa IBARA YA 54 ya kanuni ya umoja wa vijana toleo la 2017

Mgeni rasmi alikua ni mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa (NEC) Ndugu Theresia Mtewele

Mgeni rasmi amewaasa vijana kujenga umoja na mshikamano ili kuhakikisha wanatimiza shabaha na malengo ya kikanuni ya UVCCM.

Mgeni rasmi pia alisisitiza vijana kutumia fursa zilizopo kama vile, kilimo, misitu na utalii ili kujiimarisha kiuchumi.

Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi wilaya ya Mufindi, Comrade Daud Yassin Mlowe aliwataka vijana kuimarisha jumuiya ngazi ya kata na matawi ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinaendelea kuimarika kwa upande wa vijana.

Lkn pia Viongozi mbalimbali walihudhuria baraza hilo kama ifuatavyo,

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi.

Mh. Festo Elia Mgina

M/kiti wa wazazi
ndugu, Festo kilipamwambu

M/kiti UVCCM Iringa DC
Ndugu Jumah Mapesa Makalla na viongozi wengne wengi

Imeandaliwa na idara ya hamasa na chipukizi
uvccm wly ya Mufindi

Hakuna maoni: