Dstv Tanzania

MKUU WA WILAYA YA LUDEWA APOKEA BOX 7 ZA CHAKI KUTOKA STAMBULI MEDIA ZILIZOCHANGWA NA WADAU WA STAMBULI MEDIA.

Mkurugenzi wa Mtandao huu  Titho Stambuli Akimkabidhi Box la Chaki Mkuu wa Wialay ya Ludewa Mh.Edrea Tsere
Na.Titho Stambuli.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amepokea chaki Box saba zenye thamani ya shillingi 280,000/=,kutoka kwa msimamizi wa stambuli media Ndg Titho Stambuli zilizochangwa na mdau wa stambuli media na watumiaji wa mtandao huo. 

Stambuli media tumejipambanua kwajili ya usambazaji wa taarifa na kwasasa tumepiga hatua kwa kuzidi kutoa huduma kwa jamii na sasa tumeanza kutoa na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutumia sauti tuliyoipata. 

 Msimamizi wa mtandao huo Titho Stambuli amesindikizwa na katibu mwenezi mkoa wa Njombe Erasto. Ngole,Melickius moshwe, Baraka Haule, na katibu hamasa na chipukizi Mkoa Johson Mgimba.

"Mh mkuu wa wilaya tunaomba upokee chaki hizi zimechangwa na wadau wa mtandau wa stambuli media tunaomba upokee lengo letu ni kuunga mkono juhudi za kuinua elimu wilayani ludewa, sisi ni marafiki wa elimu kwani tunatambua thamani ya elimu wilayani Ludewa "

Naye mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Adrea Tsere  amepokea chaki kwa niaba ya wananchi na wadau wa elimu, ametoa shukrani za dhati  kutoka kwa wadau wa stambuli media, "Mungu awaongezee pale mlipopunguza kwa kuwa mmesaidia jamii na mnaunga mkono hatua za maendeleo ya Ludewa ".

Amesoma mbele ya watu  wote barua ya kukabidhiwa chaki na list ya majina ya watu waliochangia chaki hizo kama ishara ya kupokea kiofisi chaki hizo.

Wananchi wa Ludewa wamepongeza jambo hilo na kuahidi watazidi kufanya kazi na mtandao huo kwa kuwa kazi nzuri imeonekana na ya mfano wa kuigwa.


Hakuna maoni: