UVCCM NJOMBE WATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA MSIBA WA MAMA MZAZI WA MKUU WA MWILAYA NJOMBE RUTH MSAFIRI.
Na.Erasto Mgeni
Ni Taarifa za Huzuni na Majonzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe
Mh.Ruth Msafiri ambaye amefiwa na mama yake mzazi.
Taarifa zinasema kuwa mama mzazi huyo ambaye alikuwa
akiuguzwa na mwanae ambaye ni wa Mkuu wa
wilaya ya Njombe mwili wake umehifadhiwa
Nyumbani kwao Katoke wilayani Muleba.
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe kupitia
kwa katibu wake Sure Mwasanguti Unatoa Pole kwa Msiba ambao umefikia mkuu wa
wilaya ya Njombe Ruthi Msafiri pamoja na kumuombea Mwenyezi Mungu amtie Nguvu
katika Kipindi Hiki Kigumu.
Akizungumza na Mtandao huu Katibu huyo amesema kwa kwa
pamoja wanaungana na Mkuu wa wiliya ya Njombe katika Kuomboleza Kifo cha mama
yake mzazi.
“umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Njombe tunamtakia uvumilivu na
subira katika kipindi hiki kigumu na tunaendelea kumuombea”amesema Mwasanguti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni