VYUO VIKUU VIWE NA BODI ILI KULINDA MASLAHI YA WANAFUNZI NA WAHADHIRI
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE
wa Manonga Mh. Seif Gulamali amependekeza kuwepo kwa bodi maalumu
itakayowaongoza wahadhiri wa vyuo vikuu kiutendaji na kinidhamu.
Akichangia
katika mjadala wa kupitisha muswada wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kuhusiana na uanzishwaji wa bodi ya kitaalamu ya walimu nchini
ambayo itakuwa na majukumu ya kuinua viwango vya utaalamu wa Ualimu kwa
lengo la kuhakikisha walimu wanakuwa na viwango stahiki kitaaluma na
kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya ualimu. Gulamali amesisitiza
kuwa muswaada huo umechelewa kwani nchi kama Ghana, Kenya na Afrika
kusini zilisha kuwa na bodi za namna hiyo.
Gulamali
ameunga mkono muswada huo na kuongeza kuwa isiwe kwa walimu pekee bali
ilenge kwa wahadhiri pia ambao wana wana umoja wao kama UDOMASA kwa
wahadhiri wa Chuo kikuu cha Dodoma na UDASA kwa chuo kikuu cha Dar es
saalam.
Ameeleza kuwa
vyuo vyenye umoja huo lazima kuwe na bodi moja ambayo itawaongoza na
majukumu ya bodi iwe ni pamoja na kusajili wataalamu hao kwa ngazi za
shahada, uzamili na uzamivu na kujua idadi yao ili kuweza kuwa na
takwimu sahihi za idadi ya wataalamu hao.
Pia
ameshauri kuwa bodi hiyo iwe na kazi ya kutambua uwezo wao kitaalama
sambamba na kusimamia nidhamu hasa malalamiko ya wanafunzi hasa wakike
juu ya wahadhiri kwa manyanyaso ya kijinsia.
Aidha
amesema kuwa bodi hizo zitakuwa na maslahi kwa pande zote mbili
wawezeshaji na wawezeshwaji katika elimu ili kuweza kuzalisha wataalamu
wengi na bora zaidi.
Muswada
huo uliopita Bungeni utawalenga walimu katika ngazi zote waliohitimu
katika vyuo vinavyotambulika kwa ngazi ya Shahada, stashahada na
astashahada na utashirisha taasisi na wizata mbalimbali zikiwemo
Utumishi wa Umma, Chama cha Walimu, Maafisa elimu, Wizara ya mambo ya
ndani na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni