Dstv Tanzania

WAFANYABIASHARA WA KUSINDIKA VYAKULA MKOA WA NJOMBE WAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA VIFUNGASHIO SAHIHI

Na Elizabeth John,Njombe

Wafanyabiashara wadogo wanaosindika bidhaa za vyakula mkoani NJOMBE wamesema wanakabiliwa na changamoto ya vifungashio sahihi vya bidhaa zao hali inayokwamisha ushindani wa bidhaa zao sokoni.

Hayo yameibuka mkoani Njombe katika mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini TFDA ambapo imeelezwa kuwa wasindikaji wadogo mkoani humo wanachangamoto ya ubora wa bidhaa kutokana na kutozingatia sheria, ambapo wasindikaji hao wamesema hali hiyo inasababishwa na ukosefu wa mitaji ya kutosha katika uzalishaji na vifungashio.

Kaimu Mkurugenzi Usalama wa Chakula TFDA Jastin Makisi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanalinda usalama wa mlaji.

Aidha akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiwahakikishia wajasiriamali mkoani humo uwepo wa soko la uhakika la bidhaa wanazozalisha.

Hadi sasa TFDA wamefikia mikoa 22 kwa ajili ya kuwapa elimu ya usalama na ubora wa vyakula wakishirikisha taasisi mtambuka zikiwemo TBS, BRELA na SIDO.

MWISHO.

Hakuna maoni: