KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE AAGIZA UONGOZI WA SERIKALI KUTAFUTA SULUHU YA WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA WAKIWA SHULE
PICHANI: Katikati ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole, kulia ni Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM Mkoa wa Njombe Lucas Nyanda na Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekonadari Maheve Mr.Kitalika wakielekea jukwaani.
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe amewataka
viongozi wa Serikali na jamii kutafuta suluhu ya wanafunzi wanaopata Mimba wakiwa Shuleni. Pia amesema wote wanaodiriki kuwapa mimba wanafunzi lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria kwani hawana nia njema na watoto wa kike. Haijalishi ni wanafunzi wenzao au wanakijiji.
Ameyasema hayo katika mahafali ya Kidato cha nne iliyofanyika leo tarehe 26/10/2018 katika Shule ya Sekondari Maheve iliyoko Halmashauri ya Mji Njombe.
PICHANI: Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe akikagua wanafunzi wa Skauti.
PICHANI: Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Njombe Lucas Nyanda akisalimia wahitimu na wageni waalikwa.
PICHANI:Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe ambaye ndiye mgeni rasmi akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Maheve.
Mgeni rasmi akijibu Risala zilizowasilishwa mbele yake, katika kutatua changamoto ametoa fedha za Kitanzania kiasi cha Shilingi laki tano (500,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa blaro la chakula.
Vivyo hivyo kwa kutambua mchango wa Walimu amewapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya kwa kuwapa kiasi cha Shilingi laki Moja (100,000/=)
Lakini pia ametoa kiasi cha Shilingi laki moja (100,000/=) kwa ajili ya wanafunzi wa Skauti, amefanya hivyo kwa kutambua mchango wao katika ulizi na usalama kwa mazinmgira ya Shule.
Mkuu wa shule ametoa shukrani kwa Mgeni rasmi kwa mchango wake mkubwa, anaamini baadhi ya changamoto zitakuwa zimepatiwa ufumbuzi.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni