MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD MWALONGO AMEKABIDHI MEZA MOJA NA VITI KWENYE OFISI YA KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE
Pichani ni viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe, Kushoto kabisa ni katibu wa Jumuiya ya wazazi Lucas Nyanda, anayefuata toka kushoto ni katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akitoa shukrani kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mh. Edward Mwalongo, leo mapema tarehe 26/10/2018 amemtuma katibu wake kukabidhi meza moja na viti vitatu katika ofisi ya Katibu wa Siasa na uenezi CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole.
Katika makabidhiano hayo katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima amepokea na kutoa Shukrani za pekee kwa Mbunge, amesema anaomba na wengine wajifunze kutoa ili kuweza kukiimalisha chama cha mapinduzi.
Mwisho katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Ngole, ameomba wampelekee Mh.Mbunge shukrani za dhati na zapekee kwani amefanya jambo kubwa na la kihistoria katika ofisi yake.
Katibu wa CCM akitoa shukrani za dhati kwa katibu wa Mbunge wa Jimbo la Njombe Edward Mwalongo kwa kitendo cha kukabidhi meza na viti vitatu.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni