Dstv Tanzania

VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAKIFANYA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA MJI MWEMA MAKAMBAKO BAADA YA DIWANI HUYO ALIYEKUWA WA CHADEMA KUJIVUA




Viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Njombe wakiongozwa na katibu wa CCM (M) Paza Mwamlima na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ambao ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (M) Lucas Nyanda na Katibu wa UVCCM (M) Sure Mwasanguti wameungana na katibu wa CCM (W) Anthony Katani leo mapema wameanza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa kata ya Mjimwema Makambako ambayo ilikuwa ya CHADEMA chini ya Diwani Nolasco Mlowe.

Nolasco alijivua udiwani miezi michache iliyopita na kujiunga na CCM, na kuahidi kufanya kazi pamoja na viongozi wa CCM na wananchi ili kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kwa asilimia mia moja.

Na Erasto Kidzumbe
0753580894









Hakuna maoni: