KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI MKOA WA NJOMBE JOHNSON MGIMBA AWAAGIZA WAZAZI KUUNGA MKONO DHAMIRA YA SERIKALI KUFUFUA ELIMU TANZANIA
Pichani ni katibu wa Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Njombe Johnson Mgimba
Wazazi tuunge Mkono dhamira ya Serikali
kuifufua Elimu Tanzania jitihada za serikali tunaziona tuwaache walimu
wawe busy na kile walichotumwa kuwafundisha Watoto wetu majukumu mengine
ni yetu tuyatimize, ameyasema haya katika Mahafali ya kidato cha Nne 2018 Secondary ya Mundindi Ludewa.
Katika Changamoto zote mmezisema ameomba waanze na Jiko pamoja na Bwalo la chakula Mgimba natoa saruji mifuko 100 na ameomba kuungwa mkono na wadau wengine wote waliohudhuria mahafari hayo.
Amewaomba wanafunzi wanaobaki waache kuwa na Viburi kwa
walimu kwani kuna uhusiano mkubwa wa nidhamu na ufauru wa kitaaluma.
Amewaomba wanafunzi wanaoenda kufanya mitihani yao ya mwisho, wakienda vijijini wasiende kubweteka na kujiona kama mmeshamaliza dunia hapa mlipofikia ni sehemu ndogo sana kwanza miaka 5 ijayo huko mbeleni Form four inaenda kuwa ni Elimu ya Msingi kwa kila Mtanzania so Mawazo yenu iwe ni kwenda mbele zaidi kielimu.
Mwisho amewashukuru wote waliomuunga Mkono katika
Harambee yetu ya ghafla kuhusu ujenzi wa jiko na Bwalo vimepatikana vifaa vya ujenzi kama ifuatavyo.
1.Saruji Mifuko 250
2.Mabati 100
3.Mbao za kupaulia jiko lote
4.Shamba la miparachichi eka mbili
2.Mabati 100
3.Mbao za kupaulia jiko lote
4.Shamba la miparachichi eka mbili
Mwisho niwahakikishie wana jumuiya ya Mundindi Jengo hili
nitalisimamia kwa ukaribu Mimi Mwenyewe Mwakani tuwe tumejitoa kwenye
hili Tatizo Mgima amesema haya akihitimisha.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni