MWENYEKITI WA CHADEMA KATA YA MJI MWEMA NJOMBE MJINI BARAKA KIVI AJIUNGA NA CCM, AMECHOKA NA MATESO YALIOKO CHADEMA
Baraka Kivi ametoa kofia yake ya CHADEMA na kuvaa kofia ya CCM huku akiwa na furaha na na amesema sasa inatosha maana ameteseka vya kutosha akiwa CHADEMA
Viongozi wa kata na Mkoa wameshiriki kikao na kumpokea aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Mji mwema Baraka kivi, viongozi wa Mkoa walioshirkiki ni : katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto G.Ngole, Katibu wa jumuiya ya wazazi Lucas Nyanda na Mjumbe wa baraza kuu la wazazi Mkoa Nathanael Maxona
Mwenezi akitoa hobuba katika kikao cha kata ya Mjimwema
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe mewapongeza wanachama wa kata ya Mjimwema kwa kufanya kazi kwa bidii, ndio maana wapinzani wanaomba kurudi CCM kila siku.
Kwa sasa chama cha mapinduzi kinapokea maombi mengi sana toka kwa wanachama wa CHADEMA
wanataka kurudi CCM lakini CCM haipokei wanachama akama njugu, hivyo kunautaratibu hivyo niwaombe wanachama wanataka kurudi wafuate utaratibu.
Ukweli ni kwamba kwa sasa TZ kitabaki chama kimoja kwani vyama vingine
vimeshindwa kufanya siasa na wamekuwa ni watu wa kupinga kila kitu. Pia amewaomba wanachama kuhakikisha viongozi
wanakuwa sehemu ya jamii, na watumia fulsa kubwa walionayo kwani wako kwenye uso wa Mkoa wa Njombe.
Pia amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya Mji mwema kuhakikisha wanajenga ofisi ya kata nzuri na ya kisasa. Amewaomba wakishaweka mpango mkakati wa kujenga ofisi hiyo ya kata wafike ofisini kwa Mwenezi atatoa mifuko ya saruji mia moja (100)
Katika kikao hicho ametoa shilingi elfu hamsini (50,000/=)kwa ajili ya chaula wa wajumbe wa kikao.
Mwisho Wana CCM muda wa kuifurahia nchi yao umefika na hivyo wakae kwa amani na kuendelea kufanya juhuzi za maendeleo ya nchi.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Njombe Lucas Nyanda akitoa salaamu na kutambulisha viongozi wa Mkoa
Mjumbe wa Baraza kuu wazazi Mkoa
Nathanael Maxona akitoa salamu
Nathanael Maxona akitoa salamu
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni