Dstv Tanzania

KATIBU WA CCM MKOA WA NJOMBE PAZA MWAMLIMA PAMOJA NA SEKRETARIETI AMEMALIZA ZIARA YA MKOA WILAYANI MAKETE


Pichani ni katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima akivalishwa skafu na Greenguard

Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima pamoja na wajumbe wa Secretarieti ya Mkoa, ambao ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa Erasto Ngole, Katibu wa UVCCM Mkoa Sure Mwasanguti, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Lucas Nyanda  na Katibu wa UWT Mkoa Angel Milembe.

Katibu wa CCM Mkoa wa amemalizia ziara ya Mkoa Wilayani Makete jana tarehe 15/10/2018, katika ziara hiyo amefanya kikao na wajumbe wa Secretarieti ya Wilaya na wakuu wa Idara Halmashauri ya Makete

Katibu amewaomba wana CCM  na watumishi wa serikali kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uchumi imala wa Chama na Serikali

Pia ameomba viongozi wa chama na Serikali  kuhakikisha ilani ya Chama cha mapinduzi inatekelezwa, kwa kutekeleza ilani ya chama kero za wananchi zitakuwa zimepata ufumbuzi.

Paza ameomba watumishi wote kuhakikisha wanawajibika katika majukumu yao yanayo wahusu bila kusimamiwa na mtu na ukiona unatimiza majukumu yako mpaka usimamiwe ujuwe wewe kwa uongozi wa awamu ya tano hufai katika nafasi hiyo.

Hata hivyo amewaomba watumishi wa Chama kufanya kazi kwa kujitolea kwani chama hakina hela za kuwalipa wote wanaofanya kazi, chama kinahitaji watu wazalendo.
Katibu amewaasa wanachama kutokuwa na makundi, sisi wote ni watanzania na chama ni kimoja makundi yanatoka wapi hivyo ukiona unamakundi ujitathimini na ujue wewe kwenye chama hufai kwani makundi yanarudisha maendeleo nyuma.

Na Erasto Kidzumbe 
0753580894

















Hakuna maoni: