Dstv Tanzania

KATIBU WA CCM MKOA WA NJOMBE WA NJOMBE PAMOJA NA SECRETARITI YAKE WAFANYA ZIARA WANGING'OMBE




Pichani ni katibu wa CCM (M) Paza Mwamlima wa pili toka kushoto, akiongozana na wajumbe wa Secretarieti Mkoa wa Njombe wakipata historia ya Msitu wa Nyumbanitu

Wamepata historia hiyo waliposimama na wakiwa wanaelekea Wilayani Wanging'ombe

Pichani ni katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima akitoa hotuba Wanging'ombe

Pamoja na shukrani nyingi za katibu amewaomba wanawanging'ombe wasimamie amani na kutumia lugha moja kwa makabila yote.

Kwani mujiza mkubwa duniani pote hata nchi zilizoendelea zinashangaa kwa nchi nzima kutumia lugha moja hiyo tunu tuliopewa na Mwl. lazima tuisimamie.


Lengo kuu la chama chetu cha CCM ni ushindi chaguzi zote na kwa Wanging'ombe hakuna shaka kwani vijiji vyote ni CCM isipokuwa kijiji Kimoja.
Ili kuendelea kushinda vizuri mambo yafuatayo yazibgatiwe.
1.Kujua na kutatua kelo za wananchi
2.Kuhakikisha kwenye eneo lako unawanachama  
  wengi zaidi ya nusu ya wapiga kura ili 
  ushinde
  kirahisi
3.Kuteua wagombea wanaotokana na watu.
4.Chama kujitegemea kiuchumi, chama  
 kuombaomba sio heshima na ni aibu kila  
 ngazi  ijenge uchumi wake.
5.Mshikamano wa chama na serikali wakati wa 
 kazi na nje ya kazi.(Serikali ni chombo cha 
 CCM  cha   kufanyia kazi)
6.Katibu wa Vijana awe karibu na fulsa za 
  serikali zilizopo kwenye halmashauri.
7.Fulsa zilizopo Serikali ziwafikie vijana 
  kwa wakati
8 Kuongeza wanachama, Mkoa wa Njombe iingize 
  wanachama wengi ikiwezekana wote wawe wana 
  CCM.
8.Maendeleo ya wananchi yaendane na mafanikio ya kila kaya.
Mwisho amesema uhai wa chama ni kadi na sio nguo kwani nguo ni itikafi za uenezi tu.



















Na Erasto Kidzumbe
0753580894

Hakuna maoni: