*TAARIFA KUTOKA DAWATI LA UONGOZI WA MDA*
13/10/2018
Ndugu wanachama na wadau wa maendeleo ya Makete, hivi
karibuni MDA ilipokea mwaliko kutoka Shule ya Sekondari ya Mang'oto, ili
kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya wanafunzi kuhitimu kidato cha nne
mwaka 2018.
Katika sherehe hiyo MDA iliwakilishwa na Katibu wake Bw.
Award Mpandila. Pamoja na matukio mengine, sherehe hiyo ilikuwa na
uzinduzi wa bweni ambalo MDA imeshiriki kulijenga, kwa kushirikiana na
wananchi pamoja na wadau wengine wa maendeleo. Bweni hilo limepewa jina
la MDA.
Ujumbe muhimu uliotolewa kwa wanafunzi wanaomaliza kidato
cha nne na ambao wanaendelea na masomo ni kuwaasa waendelee kujituma,
kuwa waadilifu, kuwa na nidhamu na ari ya kujiendeleza ili waweze
kufanikiwa, kuwa mfano bora na kuliletea sifa na maendeleo taifa letu.
Sherehe hiyo imefanyika kwa mafanikio makubwa. Pia sherehe hii imetumika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu MDA.
*IMETOLEWA NA UONGOZI WA MDA*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni