VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WATEMBEMBELEA SHAMBA LA PARACHICHI LA KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE "SHIKAMOO PARACHICHI"
Pichani ni katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima akiambatana na katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti na Katibu wa jumuiya ya wazazi Lucas Nyanda, alipotembelea shambaa la Parachichi la Erasto Ngole (Shikamoo Parachichi)ambaye ni katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe
Viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe wamefika shambani kwa Katibu wa siasa na ueunezi Mkoa wa Njombe kujifunza fulsa ya kilimo cha parachichi.
Wamempongez katibu huyo kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kilimo cha parachichi na jinsi anavyowashawishi wananjombe kulima parachichi.
Hata hivyo katibu wa CCM Mkoa wa Njombe ameonyesha kushawishika na kilimo hicho kwani ni moja ya kilimo chenye faida kubwa na faida hiyo ni ya muda mrefu.
Viongozi wa CCM wamepata fulsa ya kutembelea vitaru mbalimbali ya vya miche ya parachichi na kuona namna gani miche hiyo inaandaliwa na kuwa miche bora ya parachichi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni