*MNEC VITI 15 BARA THERESIA MTEWELE AKABIDHI MIFUKO 50 YA SEMENTI SHULE YA MSINGI NJIAPANDA KATA YA ISAKALILO*
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa viti 15 Bara Bi Theresia Mtewele amekabidhi mifuko 50 kwa waalimu wa Shule ya Msingi Njiapanda iliyopo kata ya Isakalilo na kuwataka waalimu hao kuanza ukarabati wa madarasa ambapo wanafunzi wengi wanasoma mahala pasipo kuwa salama.
MNEC ametekeleza ahadi hiyo aliyoitoa wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba aidha aliwaasa waalimu hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza ufaulu mkubwa wa wanafunzi na Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwasaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo Na aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi kujenga na kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
MNEC amesisitiza walimu wafanye kazi kwa bidii na Chama Cha Mapinduzi kipo bega kwa bega kuhakikisha mazingira yao yanazidi kuboreshwa.
Katika makabidhiano hayo MNEC aliongozana na Viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Iringa ambao ni Mwenyekiti wa UVCCM MKOA Ndugu Kenani Kihongosi na Katibu SENET I na Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Mkoa Iringa Ndugu Shaibath Kapingu .
*Imetolewa na*
*Idara ya Hamasa na*
*Chipukizi Mkoa wa Iringa*
25.10.2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni