Dstv Tanzania

KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AWAOMBA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA ELIMU




PICHANI: Katikati ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole.

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe  amewaomba wazazi kuwekeza katika Elimu.Kwa kwakuwaeleza kuwa Elimu ni gharama lakini ndio urithi pekee uliobaki katika karne hii ya 21

Ameyasema hayo katika sherehe ya mahafali ya 19 ya Kidato cha nne iliyofanyika leo tarehe 30/10/2018 katika Shule ya Sekondari Ludewa iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.



PICHANI: Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe akielekea jukwaani.




PICHANI: Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Njombe  Lucas Nyanda akisalimia wahitimu na wageni waalikwa.


PICHANI:Katibu wa Siasa na Uenezi CCM  Mkoa wa Njombe ambaye ndiye mgeni rasmi akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Ludewa.


Mgeni rasmi akijibu Risala zilizowasilishwa mbele yake, katika kutatua changamoto ametoa  Mifuko mia moja(100) ya saruji  yenye thamani ya shilingi Milioni Moja na laki tano, kwa ajili ya ukarabati wa majengo yaliyochakaa.

Kwa kutambua mchango wa Walimu amewapongeza  kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulea na kuwafundisha watoto wa jamii ya Ludewa kwa kuwapa kiasi cha Shilingi laki Moja (100,000/=)


Mkuu wa shule ametoa shukrani kwa Mgeni rasmi kwa mchango wake mkubwa wa kuhakikisha wanaludewa kero zao zinatafutiwa ufumbuzi.


 
 PICHANI: Mwenezi amefika kata ya Lupingu na kujionea fulsa na changamoto za maisha.


Mwenezi akizungumza na katibu wa Jumuiya ya Vijana Wilaya ya Ludewa Hassan Kapolo.
 
 Na Erasto Kidzumbe
0753580894

Hakuna maoni: