MNEC THERESIA MTEWELE AFUNGUA SHINA LA WAKELEKETWA UVCCM KATIKA KIJIJI CHA DULAMU WANGING'OMBE
PICHANI: MNEC Theresia Mtewele akifungua shina la wakeleketwa UVCCM katika kijiji cha Dulamu Wangingombe.
PICHANI: MNEC Theresia Mtewele akipandisha Bendera baada ya kufungua shina la wakeleketwa UVCCM katika kijiji cha Dulamu Wangingombe.
MNEC ameongozana na Mwenyekiti UVCCM Mkoa, kaimu katibu wa UVCCM Mkoa na Mwalimu wa Mfunzo ya Greenguard Mkoa.
MNEC amewaomba vijana wa Kijiji cha Dulamu kuhakikisha shina linakuwa chachu katika kukijenga chama.Pia MNEC amekubali ombi la kuwa mlezi wa shina hilo ili kuweka ustawi katika shina la wakeleketwa na kuwa shina lenye tija katika Kijiji cha Dualamu.
MNEC amewaomba vijana wa Kijiji cha Dulamu kuhakikisha shina linakuwa chachu katika kukijenga chama.Pia MNEC amekubali ombi la kuwa mlezi wa shina hilo ili kuweka ustawi katika shina la wakeleketwa na kuwa shina lenye tija katika Kijiji cha Dualamu.
Pamoja na kuwa Mlezi wa shina hilo amechangia kiasi cha fedha shilingi laki moja (100,000/=)kwa ajili ya kununua kadi ili kuweza kuongeza wanachama.
Amewakumbusha Vijana kufanya kazi kwa bidii ndiyo njia pekee ya kuweza kupata mafanikio ya halali,pia amewaomba kutumia fulsa ya kilimo cha chakula ikiwemo Alizeth ili kupata Mali ghafi ya kuhudumia kiwanda kilichopo Kijijini hapo,kwani ni moja ya fulsa kubwa iliyopo katika wailaya ya Wanging'ombe.
MNEC
amefanikiwa kufungua kambi ya Vijana inayofanyika Wilayani
Wanging'ombe, ametatua kero moja ya ofisi ya Vijana kwa kutoa fedha
kiasi cha shilingi laki saba (700,000/=) kwa ajili ya kununua Computer
na vifaa vya Michezo.
PICHANI:MNEC akiwa pamoja na viongozi wa chama Wilaya na Mkoa pamoja na vijana waliofika kwa ajili ya kuanza mafunzo.
Akifungua kambi amewambia vijana ndo nguzu kazi wa Taifa letu hivyo ni lazima kufanya kazi kwa bidii,pia lazima watambue ndio viongozi wajao wa nchi hii. MNEC amewaasa vijana kujitambua na kutumia fulsa zote zinazo wazunguka ili kuweza kujipatia maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla.
MNEC akiwa na katibu wa chama Wilaya aliyesimama kulia Bi.Agness Kasela na Kushoto ni Mh.Diwani Vumi
Mwisho amewaomba Vijana kuwa wavumilivu na kushiriki shughuri zote za chama kwani chama ndio kinachoshughurikia matatizo ya wananchi wote bila kujali mwananchi huyo ni wa chama gani.
MNEC akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa Shina ikiwa ni sehemu ya uzalishaji wa kiwanda cha kijana ambaye anatoa ajira kwa vijana wenzake.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Wanging'ombe Michael Vidoga amewataka Vijana wa Wilaya hiyokuwa wasikivu kwa watoa mada ili waweze kuiva kiitikadi na maarifa na hatimaye kuwa mabarozi wazuri katika kata zao. Viongozi wengine waliokuwepo ni katibu wa CCM Wialay ya Wanging'ombe Bi.Agness Kasela, Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya, viongozi wa jumuiya nyingine za chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wanging'ombe na Mheshimiwa Diwani.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni