Dstv Tanzania

KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AMEHITIMISHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI YALIYOKUWA YANATOLEWA NA KAMPUNI YA SHEHENA MKOANI NJOMBE

 PICHANI:Katibu wa siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akifunga semina ya wajasiliamali Mkoani Njombe. 

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole amefunga semina ya usajiliamali  iliyokuwa inaendeshwa na SHEHENA GENERAL SUPPLIES CO.LTD katika ukumbi wa TURBO Njombe iliyokuwa na wananchi zaidi ya mia tatu

Amewaomba sana wananchi wote waliopata fulsa ya kujifunza wakayatumie mafunzo hayo.
Katika kufunga semina amewaambia mabinti wasifikirie suala la kuolewa kwani hawakuzaliwa ili waolewe ila amewaomba wakatafute pesa kwani heshima watapata tu hata kama hawajaolewa.
Amewashauri wana Njombe kufanya yale wanayofundishwa kwani ndio njia pekee ya kufanikiwa.

Hata hivyo amesema ujasiliamali ni rahisi sana kama kweli mtu amedhamilia na kufanikiwa kunakuja kama kweli mtu anadhamila.
Amewapongeza sana wataalamu wa SHEHENA kwa yale waliofundisha kwani wamefundisha yale yote yanayoweza kufanyika Njombe na yakawa na tija.
Katibu amesema kwa Kijana au Mwananchi wa Njombe ambaye anaishi chini ya shilingi elfu moja kwa siku huyo ameamua na anapenda kuishi hivyo kwani fulsa ni nyingi na utapatikanaji wa fedha ni rahisi ukifananisha na Mikoa Mingine. Amewakumbusha fulsa ya Liganga na Mchuchuma katika Mkoa wa Njombe hivyo wananjombe wanatakiwa kujiandaa na fulsa hiyo na wasipo jiandaa watakuja watu toka sehemu nyingine na kuchangamkia fulsa hiyo ili hali wanajombe mpo.
Ametoa ushuhuda mdogo wa kuweza kuepukana na umaskini , amesema mpaka sasa anamiezi sita anafuga kuku na ndani ya miezi hiyo sita ameshatotolesha vifaranga zaidi ya mia moja ishirini na ufugaji huo alianza na kuku watano.

 PICHANI:Baadhi ya wajasiliamali wa Mkoa  wa Njombe waliopata fulsa ya kuhudhuria  Semina ya Ujasiliamali iliyokuwa inaendeshwa na Kampuni ya SHEHENA

Katibu amefurahishwa sana na mwitikio wa wajasiliamali wa Njombe, amewapongeza kwa kuwanunulia vinywaji vyenye gharama ya laki moja na nusu (150,000/=)
 PICHANI: Meneja wa SIDO Mkoa wa Njombe akiwasalimia wajasiliamali wa Mkoa wa Njombe walioshiriki Semina .

Na mwisho amewakaribisha tena wataalamu wa   SHEHENA waje tena kutoa mafunzo mbalimbali kwa mafunzo hayo yanatija na amesema wakati mwingine wakija gharama za ukumbi atazibeba yeye kwa siku zote watakazotumia ukumbi huo.

Hakuna maoni: