Dstv Tanzania

VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAMEPOKEA TAARAIFA TOKA KWA VIONGOZI WA CCM WILAYA YA MAKETE YA KWENDA KUMUONA MH.MBUNGE WA MAKETE NORMAN SIGALA

Na Maiko Luoga Njombe.

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Wamekutana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Makete katika Ofisi ya Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa njombe Ndg. Pazza Mwamlima Kisha wakapokea Taarifa kutoka kwa Viongozi wa CCM wilaya ya Makete Ambao Wanaelekea Dar es laam Kwaajili ya Kumjulia Hali Mbunge wa Makete Mh. Norman Sigala King Aliyelazwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili Akiendelea na Matibabu.

Katika kikao hicho kifupi Katibu Wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole Asubuhi hii ya Leo Amechangia Kiasi cha Tsh. 100,000/= na kuwakabidhi Viongozi wa CCM Wilaya ya Makete kupitia kwa katibu wa CCM wilaya hiyo Ndg. Lusiano Mbosa Aliyeambatana na Wajumbe wawili kuelekea Hospital ya Taifa Muhimbili.

Aidha Kikao hicho pia Kimehudhuriwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa NEC kutoka mkoa wa Njombe Ndg. Fidelis Lumato Ambae nae amechangia Kiasi cha Tsh. 50,000 kwaajili ya Safari hiyo pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Pazza Mwamlima na Baadhi ya Wajumbe wao wamechangia Kiasi cha Tsh. 50,000.

Safari ya Wajumbe watatu Kutoka Wilayani Makete kuelekea Dar es laam Imeongozwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Makete Ndg. Lusiano Mbosa aliyewahi Kukitumikia Chama cha Mapinduzi CCM Akiwa Katibu Katika Wilaya ya Ludewa ambapo Safari hiyo ni Maalumu Kwaajili ya Kumjulia Hali Mbunge wa Wilaya ya makete Mh. Norman Sigala King.
##CCM DAIMA###



Hakuna maoni: