KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AMEHITIMISHA LIGI YA MPIRA KATA YA RAMADHANI ILIYODAHMINIWA NA VIONGOZI WA CCM KWA KUGAWA ZAWADI LUKUKI
PICHANI: Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akikagua timu kabla ya kuanza fainali.
Katibu wa Siasa Erasto Ngole ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Chama ambao ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Lucas Nyanda na Katibu wa jumuiya ya Vijana Wilaya ya Njombe Daniel Mhaza na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe kuhitimisha Ligi.
PICHANI:Katibu wa siasa akimkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe BI.Mwenda
Katibu amefurahi sana kwani kata ya Ramadhani ndio kata anayoishi, kwani ligi imeisha bila malalamiko yeyote na hakuna alivyepata majeraha ya aina yeyote ile.
Pia amewapongeza wanachi wa kata ya Ramadhani kwa uwingi wa wananchi waliokuja kuangalia fainali ya ligi iliyodhamini na viongozi wa CCM.
Hata hivyo amesema katika ahadi zake hakuahidi kuwapa zawadi wachezaji bora, Mfungaji bora na Gori kipa bora ila kwa namna walivyochezea na kufunga magori na baadhi ya gori kipa kuokoa magori amewapa zawadi kwani wamecheza kwa kiwango cha juu ambacho hakufirikilia kama kuna kijana wa Ramadhani anaweza kucheza hiyo.
PICHANI:Kushoto ni katibu wa Jumiya ya Wazazi Mkoa wa Njombe Lucas Nyanda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Ramadhani
Kwa mwitikio huu wa ligi kata ya Ramadhani ameomba iandaliwe mechi Moja kati ya Vijana wa Ramadhani na Vijana wa Kibena na Mshindi atajipatia Fedha taslimu Kiasi cha Shilingi laki tano (500,000/=)
PICHANI:Katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe Daniel Mhaza akijitamnbulisha.
Amewambia Chama kinachoweza kuwakumbuka Vijana na kudhamini ligi kubwa na yenye gaharama kama hii ni Chama cha Mapinduzi tu, hakuna chama kinginge chenye uwezo huo kwani viongozi wa vyama vingie wanapigana kupata nafasi kwa ajili ya matumbo yao na Famili zao tu.
Fainali hiyo Mshindi wa kwanza amepata Kombe lenye gharama ya laki tatu (300,000/=) na jezi zenye gharama ya laki mbili na elfu sabini (270,000/=) na Mpira mmoja wenye gaharama ya laki mbili (200,000/=)
Mshindi wa pili amepata Mbuzi Mmoja mwenye gharama ya elfu themanini (80,000) na Mpira mmoja wenye gaharama ya laki mbili (200,000/=) na sabuni miche miwili yenye gharama ya shilingi (5,000) na fedha taslimu elfu therathini (30000/=)
Mshindi wa tatu amepata Mpira Mmoja wenye thamani ya shilingi laki mbili (200,000/=) na fedha taslimu elfu ishirini ( 20,000/=) na sabuni miche miliwi yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000/=)
Mshindi wa nne amepata Mpira Mmoja wenye thamani ya shilingi laki mbili (200,000/=) na elfu ishirini (20,000/=) Miche Miwili yenye thamani ya shingi elfu tano (5,000/=)
Katibu wa siasa na Uenezi amewapa zawadi wachezaji bora wa ligi hiyo akishirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Mwenda
Mfungaji bora wa kwanza amepata zawadi ya Miche miwili ya sabuni yenye thamani ya shiringi elfu tano (5,000/=) na fedha kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000/=)
Mfungaji bora wa pili, hawa walikuwa wawili wote wamepata zawadi ya Miche miwili ya sabuni na kila mmoja amepewa fedha kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000/=) kila mmoja .
Goli kipa bora amepewa Miche ya sabuni miwili yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000) na fedha taslimu shilingi elfu kumi (10,000/=)
Na mwisho ni Mchezaji bora bora amepata miche miliwi ya sabuni na yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000/=) na fedha taslimu kiasi cha shilingi elfu therathimi (30,000/=)
Mwisho ametoa kiasi cha Shilingi elfu hamsini ambayo ni zawadi kwa Mwenyekiti wa CCM kata ya Ramadhani(50,000/=, pia elfu therathini (30,000/=) kwa katibu wa UVCCM kata ya ramadahni na Elfu therathini (30,000/=) kwa Mwenyekiti UVCCM kata ya Ramadhani
SHIKAMOO CCM,
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni