Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Njombe wakiongozwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ndugu Fidelis Lumato wa tatu kutoka kwa mkuu wa mkoa pamoja na Katibu wa jumuiya ya Vijana wa CCM Mkoa wa Njombe ndugu Sure Mwasanguti waliongozana na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Njombe pamoja na Mhe Mbunge Mwalongo katika ziara hiyo. Wakati akitoa salamu za chama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ndugu Fidelis Lumato aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi. Katika hatua nyingine Mjumbe huyo wa NEC alimpongeza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe. Edward Mwalongo kwa jitihada kubwa anazozifanya ili kuwaletea maendeleo wananchi wake, amesema wananchi wa jimbo la Njombe wamepata Mbunge anaefanya kazi kwa vitendo badala ya maneno.(CCM KAZI TU, MAGUFULI KAZI TU, MHE. MKUU WA MKOA KAZI TU, MHE. MBUNGE KAZI TU) Viva CCM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni