Dstv Tanzania

VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAMEPATA SEMINA ELEKEZI NAMNA YA KUSAIJILI WANACHANA KWA MFUMO MPYA WA KIELETRONIC


Na Maiko Luoga Njombe.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kutoka Ngazi ya Taifa kwa kushirikiana na Viongozi wa Mkoa wa Njombe Leo November 07 Mwaka huu Wametoa Semina Elekezi Kwa Viongozi wa Chama hicho ngazi ya Wilaya zote Za Mkoa wa njombe Juu ya Kusajili wanachama Kupitia mfumo mpya wa Kielektronic.

Semina hiyo Elekezi Kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Imeongozwa na Ndg. Shafii Mussa Mtaalamu wa TEHAMA Kutoka Idara ya Uchumi na Fedha Makao makuu ya  Chama cha Mapinduzi CCM Ngazi ya Taifa Kwa lengo la Kuhamisha Taarifa za Mwanachama Wa CCM Kutoka Mfumo wa Zamani Analogy na Kuingia katika Mfumo mpya wa Digital.

Akizungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Shafii Mussa Amesema kuwa Usajili Mpya wa Taarifa za Wanachama Kutoka Mfumo wa Zamani wa Analogy Kuelekea Mfumo mpya wa Digital Utamuwezesha Mwanachama wa CCM Kumiliki Kadi mpya ya Chama Kupitia Mfumo mpya wa Digital Mfano wa ATM Card.

Amesema kuwa Kupitia Mfumo mpya wa Kadi ya Kielektronic Kutamuwezesha Mwanachama wa CCM Kutunza Taarifa mbalimbali za Chama na Taarifa zake Binafsi Tofauti na Ilivyokuwa Awali Kwakutumia Kadi za Karatasi Ambazo Uendeshaji wake ulikuwa na Gharama Kubwa Tofauti na Kadi mpya ya Electronic.

Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mkoa Walioshiriki Semina hiyo Elekezi nipamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Paza Mwamlima, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Njombe Ndg. Neemia Tweve, Katibu wa Jumuiya Hiyo Mkoa wa Njombe Ndg. Sure Mwasanguti Pamoja na Baadhi ya Viongozi Mbalimbali wa Jumuiya zote za CCM mkoa wa Njombe.

Kwaupande wa Makatibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kutoka Wilaya za Mkoa wa Njombe ikiwemo Wilaya za Ludewa, Njombe, Makete na Wanging'ombe Wamepongeza Uamuzi Huo wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Taifa kwakuamua Kutumia Mfumo mpya wa Kadi za Electronic kwakuwa Itamuhamasisha Kila Mwanachama Kumiliki Kadi hiyo kutokana na Umuhimu wake tofauti na Kadi za zamani zilizotengenezwa kwa Karatasi.

Hakuna maoni: