Dstv Tanzania

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA NJOMBE NAHEMIA TWEVE AWAELEZA UKWELI JUU YA MZIGO ULIOCHUKUALIWA NA RAIS KATIKA ELIMU


PICHANI:Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akihotubia katima hafla fupi ya kuhitimu Masomo PATMO centers

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve awashukia wazazi juu ya suala la Elimu akiwa kwenye hafla fupi ya Mahafari PATMO centers yenye vituo vingi na wanafunzi mchanganyiko ambao ni watoto na watu wazima

Katika hafla hii fupi napenda tuelezane ukweli kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. Magufuli imebeba mzigo mkubwa sana wa Elimu kuanzia ngazi ya shule ya Msingi hadi vyuo vikuu Mtweve amesema.

Ameomba sana wazazi na wananchi kwa ujumla kuunga mkono jitihada hizi za serikali hii.

Amesema walimu wana kazi nzito sana ni wajibu wa wazazi kuwatia moyo na hamasa ili wapate moyo wa kufanya kazi kwa weledi mkubwa.
Isiwe kwamba ukimpeleka mtoto shule ndo unakuwa umemaliza, hata kwenda kutazama maendeleo ya mtoto unakimbia kwa sababu Elimu ni bure.

Ni wajibu wetu sote kuweka mazingira bora ya elimu tanzania.

SHIME WANANJOMBE NA WATANZANIA WOTE, TUIBOTESHE ELIMU.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894

Hakuna maoni: