MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD MWALONGO AENDELEA NA ZIARA NDANI YA JIMBO
Pichani ni Mhe.Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Edward Mwalongo akiwa na Katibu Tarafa Njombe Mjini, Bi Nyemere
Mhe Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo wakiongozana na viongozi wa chama cha mapinduzi wa Wilaya ya Njombe aendelea na ziara ndani ya jimbo la Njombe mjini.
Akiwa katika mtaa
wa kibena kata ya Ramadhani ambapo amehotubia wananchi na kujibu baadhi
ya changamoto zinazowakabili.
Mbunge amesisitiza jambo la Elimu na kuwashauri wazazi kuendelea
kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao mashuleni ili kuweza kujua maendeleo ya kitalumu ya wanafunzi kwa kufanya hivyo itasaidia kuboresha
taaluma na hatimae tuweze kutengeneza taifa la wasomi na wazalendo kwa
nchi yao.
Baadhi ya viongozi wa chama alioongozana nao katika ziara yake.
Hata hivyo ameshauri wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika
kupima afya zao na kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI ili
Njombe yetu ibaki kuwa salama.
Kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunazuia kupoteza nguvu kazi yetu ya Njombe na Tanzania kwa ujumla kwani afya ndio mtaji wa kwanza katika uzalishaji.
Kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunazuia kupoteza nguvu kazi yetu ya Njombe na Tanzania kwa ujumla kwani afya ndio mtaji wa kwanza katika uzalishaji.
.
Mhe Mbunge ameahidi kuendelea kutoa
ushirikiano na kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na
miundombinu inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati ili kuweza kukidhi ahadi za Mh.Rais.
Katika hotuba yake amewaasa vijana na wananchi wote kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujipatia kipato halali kwani hakuna namna nyingine ya kupata kipato zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.
Hata hivyo amewaambia wananchi wa Njombe wanabahati kubwa kwani mkoa wa Njombe ni moja ya Mkoa wenye fulsa nyingi ikiwa kijana au mwananchi amedhamilia kufanya kazi kwa bidii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni