UWT MKOA WA NJOMBE WAADHIMISHA WIKI YA WANAWAKE KWA VITENDO
Pichani ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Bi,Rosemary Lwiva
Na Maiko Luoga Ludewa.
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania UWT Mkoa wa Njombe wakiongozwa na Viongozi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ludewa leo wamefanya Maadhimisho ya Wiki ya UWT Kimkoa katika Kata ya Luilo Wilayani Ludewa.
Jopo la Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT ya CCM Mkoa wa Njombe Bi,Rosemary Lwiva, Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa Bi,Anjela Milembe Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ludewa Bi, Leah Mbilinyi pamoja na Katibu wa UWT Wilaya ya Ludewa Bi, Frolah Kapalia Wameshiriki Shughuli mbalimbali za Ujenzi katika Kituo cha Afya cha Kata ya Luilo.
Pichani ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve
Aidha Viongozi wengine walioshiriki Maadhimisho hayo Ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Njombe Bw, Neemia Tweve, Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Njombe pamoja na Madiwani wote wa Viti maalumu kutoka katika Tarafa Tofauti za Wilaya ya Ludewa.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika Eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata ya Luilo Mbuyuni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Bi, Rosemary Lwiva Amesema kuwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Nchini Kushiriki na Wananchi katika Shughuli za Maendeleo ni zoezi Endelevu Ikiwa ni moja ya Hatua za Kuisimamia Serikali ya Awamu ya Tano katika Kutekeleza Majukumu yake.
Kwaupande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Ludewa Bi, Frolah Kapalia Licha ya Kutumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Wanachama wa CCM Kuwa ndiye katibu mpya wa UWT wilaya ya Ludewa Baada ya Bi,Maimuna Mwakaje Aliyeshika Nafasi hiyo Kustaafu Amewaomba wanachama wa CCM Kumpa ushirikiano wa Kutosha ili kukiboresha chama wilayani humo.
Baada ya Viongozi hao wa CCM Kushiriki Shughuli za Usombaji Mchanga,Kusogeza Tofali na Kuchanganya Zege Katika Eneo la Ujenzi walipata nafasi ya Kusikiliza Kero na Maoni ya Wananchi wa Kata ya Luilo ambao licha ya Kutoa changamoto zao wananchi hao pia walitumia nafasi hiyo Kutoa salamu za Shukrani kwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kwa kutoa Fedha kiasi cha Tsh,Milioni 500 kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Luilo.
Aidha Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais Magufuli imetoa Kiasi cha Tsh,Milioni 500 kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Luilo, Milioni 500 Kituo cha Afya Mlangali na Milioni 400 Katika Kituo cha Afya Manda na zoezi la Ujenzi na Ukarabati wa Vituo hivyo vya Afya katika Wilaya ya Ludewa Linaendelea kwa kasi.
picha nyingine wakifanya shughuli mbalimbali za ujenzi
picha nyingine wakifanya shughuli mbalimbali za ujenzi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni