MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI EDWARD MWALONGO ATEMBELEA KIKUNDI CHA AKINA MAMA NA KUKIWEZESHA
Mh. Mbunge wa jimbo wa Njombe Mjini Edward Mwalongo, amefanya ziara ya kutembelea kikundi cha wanawake Mtaa wa Kibena Hospitali, ameambatana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angel Mwangeni, Mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi Wilaya ya Njombe Kasanga Makweta na Katibu wa Jumuiya ya Vijana Wilaya ya Njombe Daniel Muhaza
Mheshimiwa amewapa wanakikundi hao mradi wa Nguruwe kumi na moja (11) wenye thamani ya shilingi laki sita na sitini elfu (660,000/=)
Akiwa anawakabidhi Nguruwe hao amewaomba wanakikundi hao kuboresha mradi huo ili uwe mradi wenye tija katika jamii.
Afisa mifugo akitoa Elimu namna ya kufunga Nguruwe kitaalamu
Mh.Mbunge ameambatana na afisa mifungo toka ofisi ya mbunge kwa ajili ya kutoa elimu namna ya kufuga nguruwe hao kitaalamu na sio kwa mazoea.
Licha ya elimu iliyotolewa na afisa mifugo, lakini Mbunge amemwomba afisa mifugo kuwa karibu na kikukndi hicho ili kuweza kuwasaidia kufuga Nguruwe hao kitaalamu aidha wanakikundi hao kupata ushauri wa kitaalamu.
Baadhi ya akina mama wakikabidhiwa vibwagala hao wa Nguruwe na Mh.Mbunge, pamoja na kukabidhiwa vibwagala hao wamemwomba Mheshimiwa kuendele kusaidia vikundi vingine vya akina mama ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni