Dstv Tanzania

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE AKIENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI LUDEWA AMEZINDUA SHINA LA WAKELEKETWA LA VIJANA WA BODABODA



PICHANI: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala akizindua shina la wakeleketwa la Vijana wa Bodaboda  wa kata ya Ludewa Mjini.




Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njmbe Jasel Mwamwala  akivalishwa Skafu na Greenguard wa Wilaya ya Ludewa

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe akikagua ujenzi wa Zahanati ya Ludewa  Kijijini, Mwenyekiti wa CCM amepongeza jitihada zinazoendelea katika ujenzi wa Zahanati hiyo, ameunga mkonokwa kutoa kiasi cha fedha kiasi cha shiling laki mbili na ishirini na tano elfu (225000)kwa ajili ya kununulia Saruji


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe ameungana na wanafunzi wa wa Shule ya Msingi Songambele kupata chakula cha Mchana.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe amefurahishwa na jithada za walimu  na wazazi kwa ajili ya kuandaa chakula ili wanafunzi wapate Chakula wakiwa Shuleni, kwa kufanya hivyo wanafunzi watakuwa na utulivu na kufanya wasome kwa bidii
PICHANI: Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akiwa na Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Njombe wakipata chakula pamoja na wanafunzi katika shule ya Msingi Songambele


MNEC Fedelis Lumato Kushoto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa wa pili toka kushoto wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe wakipata Chakula ambacho ndicho chakula huliwa na wanafunzi wa shule ya Msingi Songambele.

Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe
0753580894











Hakuna maoni: