Dstv Tanzania

*TAARIFA KWA VIJANA WA CCM NCHINI*



*KUTOKA DAR - ES- SALAAM*
*28/11/2018*
*Umoja wa vijana wa CCM UVCCM TAIFA* unapenda kuwatangazia vijana wote Nchini wenye nia na sifa za kugombea uongozi ndani ya *CCM*, kuwa nafasi ya *Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA (NEC) Kupitia Jumuiya ya Vijana Nafasi  tatu bara Iliokuwa ikishikiliwa na Ndugu Sofia Kizigo ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo ipo wazi* na zoezi la kuchukua na kurudisha fomu linaanza kesho *Tarehe 29/11/2018* na mwisho ni *Tarehe 30/11/2018* Saa 10 Jioni.....  Nafasi inayotakiwa kujazwa ni 1 (Moja)

Hivyo, *UVCCM* kupitia *Idara ya Oganizasheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa* inapenda kutoa wito kwa vijana wote kujitokeza na kushiriki mchakato wa uchaguzi, Fomu zitatolewa Ofisi zote za Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa pamoja na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya *UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA, Upanga- Dar es salaam*

*Asante, na Karibuni.*

*Imetolewa na*
*Idara ya Uhamasishaji na Chipukiz UVCCM TAIFA*

Hakuna maoni: